Masuala ya UM

Hongera Rais wa Somalia tutakupa ushirikiano:UN

Umoja wa Mataifa umempongeza Rais mpya wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud aliyeapishwa hii leo mjini Mogadishu nchini Somalia na kuahidi kutoa ushirikiano kwa serikali yake katika kutimiza vipaumbele vya nchi hiyo.

Vita Ukraine: Bei za nishati, chakula zazidi kupaa 

Zaidi ya siku 100 zimepita tangu Urusi kuvamia Ukraine, na hii leo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametambulisha ripoti ya pili kutoka kikundi cha kuchukua hatua dhidi ya janga la dunia litokanalo la vita hivyo, GCRG na kusema madhara ya vita hiyo katika sekta ya chakula, nishati na fedha ni dhahiri shairi na yanazidi kuongezeka kila uchao.

Csaba Kőrösi wa Hungary atakuwa Rais wa kikao cha 77 cha Baraza Kuu

Mwanadiplomasia Csaba Kőrösi atakuwa Rais wa mkutano wa 77 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Ni raia wa wa Hungary ambaye amechaguliwa kwa shangwe Jumanne hii katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa, jijini New York, Marekani. 

Ajali kwenye bohari Bangladesh yachochea ILO kusaka usalama kazini

Shirika la Umoja wa Mataifa la kazi duniani, ILO limetaka hatua zaidi zichukuliwe kushughulikia na kuhifadhi kemikali pamoja na mafunzo kwa wafanyakazi wa bohari za kemikali ili kuepusha janga lililotokea mwishoni mwa wiki huko Bangladesh kwenye bohari la kontena mjini Chattogram kusini mashariki mwa nchi hiyo.

Tunayo heshima kubwa kwa walinda amani kutokana na kujitolea kwao - Guterres 

“Leo, tunayo heshima ya kuwaenzi wanawake na wanaume zaidi ya milioni moja ambao wameshiriki kama walinda amani wa Umoja wa Mataifa tangu mwaka 1948.” Ndivyo alivyoanza Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres katika ujumbe wake wa siku ya kimataifa ya walinda amani. 

Katika siku 3 zijazo tuna fursa ya kipekee ya kutoka katika hatari kwenda kwenye mnepo - Amina J. Mohammed 

Jukwaa la kwanza la kimataifa kuhusu kupunguza hatari za majanga limeanza leo mjini Bali, Indonesia ikiwa ni fursa ya kipekee ya kuweka njia kwa "hatima salama na endelevu.” 

Kenya, WHO na Bloomberg wazindua mradi kupunguza vifo vya ajali za barabarani 

Ajali za barabarani ni sababu ya tano kuu ya vifo vya Wakenya wenye umri wa kati ya miaka 5 na 70, na ni muuaji mkuu wa wavulana wenye umri wa miaka kati ya 15-19 limesema leo shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani WHO. 

UNAIDS yaonya hatari ya unyanyapaa juu ya ugonjwa wa Monkeypox

Shirika la Umoja wa Mataifa lakutokomeza UKIMWI UNAIDS limeelezea wasiwasi wake kwamba baadhi ya ripoti na maoni yanayotolewa kwa umma juu ya Monkeypox yanatoa lugha na taswira za chuki,ubaguzi na unyanyapaa hasa kwa wa Afrika na watu wanaishiriki mapenzi ya jinsia moja LGBTI 

Hakuna nchi iliyo na kinga dhidi ya njaa, lazima tuchukue hatua sasa:UN 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameliambia Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kwamba vita vinapozuka, watu wanakabiliwa na njaa, na kwamba asilimia 60 ya watu wasio na lishe bora duniani wanaishi katika maeneo yaliyoathiriwa na migogoro huku akikumbusha kuwa "Hakuna nchi iliyo na kinga dhidi ya njaa,"  

Zaidi ya wahamiaji 1000 kutoka Afrika Mashariki wamekufa au kutoweka

Shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM limesema zaidi ya wahamiaji 1,000 wamefariki dunia au kutoweka tangu mwaka 2014 walipokuwa wakijaribu kuondoka Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika.