Licha ya mashambulizi ya wiki hii nchini Jamhurui ya Afrika ya Kati , CAR Katibu Mkuu wa Umoja wa Msataifa Antonio Guterres amesema hii leo anashikamana na taifa hilo na kuonya kwamba mashambulizi dhidi ya raia wasio na hatia wasioweza kujitetea na walinda amani wa Umoja wa Mataifa yanaweza kuwa ni uhalifu wa kivita.
Umoja wa Mataifa umetoa wito wa nchi wanachama kushikamana na kusaidia vita dhidi ya mtandao wa kigaidi wa Al-Qaeida na ISIL kwenye ukanda wa sahel barani Afrika.
Mkutano wa kwanza wa nchi wanachama wa Shirika la Uhamiaji la Umoja wa Mataifa (IOM), kuhusu mbinu jumuishi za uhamiaji na kuoanisha njia za wahamiaji kwenda Ulaya, umefanyika mjini Brussels, Ubelgiji na kuleta matumaini kwa mashirika yanaohusika na wakimbizi na wahamiaji.
Kuelekea siku ya watoto duniani tarehe 20 mwezi huu wa Novemba, mtoto muigizaji Millie Bobby Brown ameungana na mabalozi wema wa shirika la kuhudumia watoto duniani, UNICEF kutumia video mahsusi kupigia chepuo kampeni ya kusongesha haki za watoto duniani.
Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet ameitolea wito serikali ya Bangladesh kusitisha mipango ya kuwarejesha wakimbizi wa Rohingya Myanmar akionya kuwa urejeshaji huo huenda ukakiuka sheria za kimataifa za haki za binadamu na kuyaweka maisha yao na uhuru wao hatarini.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, washirika wa Umoja wa Mataifa na chama cha msalaba mwekundu nchini Syria, wamekamilisha misafara ya siku sita ya misaada ya kibinadamu kwenye kambi ya Rukban iliyoko Kusini Mashariki mwa Syria karibu na mpaka wa Jordan.
Shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM Novemba 8 mwaka huu limeanza tena mpango wa huduma ya hiyari ya safari za ndege za kibinadamu (VHR) kwa wahamiaji kwenye mji wa kusini mwa Libya wa Sebha.
Shirika la afya ulimwenguni WHO limesema mapigano yanayoendelea hivi sasa kwenye mji wa Hudaidah nchini Yemen yanazidi kuweka hatarini makumi ya maelfu ya watu na kuzuia shirika hilo kuwafikishia misaada ya dharura wanayohitaji
Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, umelaani janga la kibinadamu linaloendelea kwenye eneo la Batangafo mkoani Ouham kaskazini-maghaibi mwa nchi hiyo.
Njaa, utapiamlo, uhaba wa lishe, pamoja na utipwatipwa vinaathari kubwa kwa watu wenye kipato kidogo, wanawake, watu wa asili , wale wenye asili ya Kiafrika na pia familia zinazoishi mashambani katika eneo la Amerika ya kati na Caribbean.