Mpango mkakati wa msaada wa kibinadamu HRP wa mwaka 2019 umetoa ombi la dola milioni 350 ili kutoa huduma za msingi kama chakula, ulinzi, huduma za afya, malazi, maji na usafi kwa Wapalestina milioni 1.4 ambao wamebainika kuwa na mahitaji makubwa ya kibinadamu kwenye Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Maghariki likiwemo eneo la Jerusalem Mashariki.