Masuala ya UM

Mashambulizi dhidi ya Wapalestina lazima yakome: Krähenbühl

Shirika la  wa Umoja wa Mataifa la usaidizi kwa wakimbizi wa  Palestina UNRWA limesema lina wasiwasi kuhusu mgogoro wa kivita unaondelea kando mwa kambi ya wakimbizi wa Kipalestina  ya Yarmouk.

Wafanyakazi 10 watoweka nchini Sudan Kusini.

Wafanyakazi 10 wa kutoa misaada ya kibinadamu nchini Sudan Kusini wametoweka wakati wakiwa kwenye msafara wa kutathmini mahitaji ya kibinadammu huko Yei jimbo la Equatoria ya Kati nchini humo.

Machungu niliyopitia Libya hayafikiriki

Nimepitia machungu makubwa zaidi nchini Libya sasa nimerejea nyumbani nina imani kubwa. Hiyo ni kauli ya mmoja wa raia 121 wa Cameroon ambao wamerejeshwa nyumbani hivi karibuni kutoka Libya baada ya ndoto zao za kuelekea Ulaya kusaka maisha bora kutumbukia nyongo.

Viwango vipya vya kudhibiti wadudu wa mimea vyapitishwa: FAO

Mkataba wa kimataifa wa kulinda mimea IPPC leo umeidhinisha viwango vipya venye lengo la kuzuia wadudu waharibifu katika kilimo na mazingira kuvuka mpaka na kusambaa kimataifa.

Hakuna aliyezaliwa gaidi duniani ni mkanganyiko wa mambo:Guterres

Hakuna mtu aliyezaliwa gaidi na hakuna sababu yoyote inayohalalisha ugaidi. Hayo yamesemwa leo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika mkutano wa 16 wa bodi ya ushari ya Umoja wa Mataifa ya kupambana na ugaidi unaofanyika Saudia.

Watu zaidi ya 250 wapoteza maisha kwenye ajali ya ndege Algeria

Abiria zaidi ya 250 na wahudumu wa ndege wamepoteza maisha leo asubuhi katika ajali mbaya iliyohusisha ndege ya kijeshi nchini Algeria. 

Messi kupeperusha bendera ya utalii

Wacheza soka nao wana nafasi yao kuchagiza utalii unaojali siyo tu mazingira bali pia jamii na ndio hapo Lionel Messi anajumuika!

Asante China kwa kuendelea kutuunga mkono- Guterres

Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres akutana na Rais Xi Jinping wa China mjini Beijing.