Vyombo vya habari vimeripoti kuwa watu 66 wamefariki dunia kwenye ajali ya ndege hii leo huko Iran na tayari Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametuma salamu za rambirambi.
Baadhi ya watu wamekuwa wakidai Radio ni chombo cha habari kinachokufa , lakini ukweli ni kwamba Radio imezidi kushamiri na itaendelea kuwa chombo muhimu cha mawasiliano katika jamii ndani na nje ya masuala ya kibinadamu.
Utangazaji wa michezo kupitia redio umenisaidia siyo tu kutambulika bali pia kujifunza mengi na hivyo kuimarisha stadi zangu na kuhabarisha jamii inayonisikiliza.
Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imelaani kukamatwa kwa majaji wawili wa Mahakama Kuu nchini Maldives ikisema ni ukiukwaji wa utawala wa sheria na uhuru wa mahakama kufanya kazi katika misingi yake.
Uchangamfu wa mashindano ya olimpiki ni ishara muhimu ya amani katika dunia ya leo, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres huko PyeongChang nchini Korea Kusini kunakofanyika mashindano hayo ya majira ya baridi.
Amani ya kudumu Sudan Kusini bado ni mtihani mgumu unaohitaji juhudi za jumuiya ya kimataifa, serikali ya Sudan, pande zote kinzani nchini humo na mshikamano wa raia wote wa Sudan Kusini.