Masuala ya UM

Syria yahitaji kupiga hatua zaidi hata baada ya maendeleo kwenye afya UM

Mtaalamu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na haki ya kupata huduma za afya ameitaka Syria kufanya juhudi zaidi kuhakikisha kuwa wananchi wake wamepata huduma bora.

Kongamano kuhusu kuimarisha afya mijini laanza Japan

Wakati zadi ya nusu ya watu wote duniani wakiishi mijini viongozi kutoka seriali , wasomi , vyombo vya habari na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali wote wamekusanyika kwenye kongamano la Umoja wa Mataifa mjini Kobe nchini Japan kujadili njia za kuimarisha afya kwa wenyeji wa mijini.

Wafungwa wengine wa kisiasa waachiliwe pia Myanamar:Pillay

Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay amekaribisha kuachuachili Jumamosi jioni Aung San Suu Kyi katika siku ya mwisho ya kifungo chake cha nyumbani.

Baada ya zaidi ya muongo kizuizini Aung San Suu Kyi aachiliwa huru, Ban akaribisha hatua hiyo

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekaribisha hatua ya kuachiliwa huru kwa kiongozi anayepigania demokrasia nchini Myanmar Aung San Suu Kyi.

Siku ya ugonjwa kisukari duniani

Siku ya maadhimisho ya ugonjwa wa kisukari diniani ambayo itakuwa tarehe 14 mwezi huu inajiri wakati kukifanyika juhudi za kupambana na magomjwa sugu yanayosababisha usumbufu na kurudisha nyuma maendeleo kwenye nchi nyingi maskini duniani.

Ban ahutubia viongozi wa mataifa ya G20 kwenye siku ya mwisho ya mkutano wao

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa wito kwa viongozi wa mataifa tajiri na yale yanayoinukia kiuchumi ya G20 kulifanya suala la maendeleo kuwa muhimu.

Afrika yataka mfuko wa haki uzingatiwe kupata uwakilishi kwenye Baraza la Usalama

Nchi hizo ambazo zinaunda jumuiya ya nchi zisizofungamana na upande wowote, iliyoundwa katika miaka ya 1960 wakati kulikozuka vita baridi, zinataka kuwepo kwa mageuzi kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ili kukaribisha uwakilishi sawa wa kimabara.

Haki izingatiwe katika uwakilishi Baraza la usalama:Afrika

Nchi hizo ambazo zinaunda jumuiya ya nchi zisizofungamana na upande wowote, iliyoundwa katika miaka ya 1960 wakati kulikozuka vita baridi, zinataka kuwepo kwa mageuzi kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ili kukaribisha uwakilishi sawa wa kimabara.

Latin America yapiga hatua kubwa juu ya wakimbizi duniani

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi UNHCR limekaribisha kwa mikono miwili azimio linalotaka kulindwa na kuheshimiwa kwa wakimbizi katika eneo la nchi za Latini Amerika.

UM umekaribisha mipango ya Congo kuanzisha sheria ya kwanza Afrika kulinda watu wa asili:

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za watu wa asili ameipongeza serikali ya Jamhuri ya Congo kwa hatua kubwa inazochukua kutambua na kulinda haki za watu wa asili.