Kuelekea mwaka mpya wa 2019, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametumia salamu zake za mwaka mpya akifanya tathmini ya mwaka 2018 na matarajio yake kwa mwaka mpya.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres leo akiwa mjini New York Marekani kabla ya kusafiri kwenda Argentina unakofanyika mkutano wa nchi 20 zilizoendelea zaidi kiuchumi G20, amewaambia wanahabari kuwa changamoto kubwa hivi sasa ni ukosefu wa kuaminiana duniani.
Kila siku ajali za barabarani hukatili uhai wa maelfu ya watu, kuwaacha wengine na ulemavu wa maisha na kuathiri mustakhbali wa familia nyingi duniani. Na wakati wa kuchukua hatua dhidi ya zahma hiyo ni sasa limesema shirika la afya duniani, WHO.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan, Mohamed Ahmed Eldirdiri amehutubia mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na kusema kuwa mazingira ya sasa yanatia moyo katika kupatia suluhu masuala yote yaliyosalia kati ya nchi yake na Sudan Kusini.
Taka zilizokithiri katika makazi ya binadamu ni lazima zidhibitiwe la sivyo zitaweka hatarini sio tu mazingira bali afya zao. Wito huo umetolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la makazi UN-HABITAT hii leo katika kuadhimisha siku ya makazi duniani.
Misingi mikuu mitatu ambayo ni uongozi bora, kushirikiana majukumu na kuchukua hatua za pamoja ni muhimu kwa mustakhbali wa dunia amesema Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Maria Espinosa.