Masuala ya UM

John Holmes, Mkuu wa OCHA ameanza ziara ya siku tisa Afrika

Naibu KM juu ya Misaada ya Dharura, John Holmes ameanza ziara ya siku tisa Afrika na alitazamiwa kuzuru Ethiopia, Sudan na Kenya. Holmes atakutana kwa mashauriano na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa yanayohudumia misaada ya kiutu pamoja na maofisa wa UM, na pia wanadiplomasiya waliopo kwenye nchi anazozuru kushauriana juu ya hatua zinazofaa kuchukuliwa shirika, ili kuwanusuru kimaisha mamilioni ya watu walioathirika kihali kutokana na mifumko ya vurugu liliotanda kwenye maeneo yao katika siku za karibuni.

Waalimu wa kazi za polisi wa UM wapelekwa Chad

Kundi la mwanzo la maofisa watano wa polisi kutoka Kitengo cha UM kinachohusika na Ujenzi wa Huduma za Dharura za Polisi (SPC) limepelekwa Chad wiki hii kuanzisha mafunzo maalumu ya polisi wa kuhudumia ulinzi na usalama wa wahamiaji wa ndani ya nchi 300,000 pamoja na wahamiaji wa kutoka eneo jirani la Darfur, Sudan walioathiriwa na hali ya mapigano.

Mjumbe Maalumu mpya wa KM kwa Cote d'Ivoire ameanza kazi

Mjumbe Maalumu mpya wa KM kwa Cote d’Ivoire, Choi Young-Jin amewasili nchini humo mapema wiki hii kuanza kazi. Choi ameahidi kushirikiana na makundi yote ya kisiasa yanayoanmbatana na mgogoro wa Cote d’Ivoire, bila ya upendeleo, ili kuhakikisha amani inaimarishwa nchini pote kwa masilahi ya umma kijumla.

Hali Usomali inawatia wasiwasi mkubwa wajumbe wa Baraza la Usalama

Baada ya mashauriano kukamilishwa ndani ya Baraza la Usalama juu ya hali katika Usomali, Balozi Marty Natalegawa wa Indonesia, Raisi wa Baraza kwa mwezi Novemba, aliwasilisha kwa waandishi habari taarifa ya pamoja, kwa niaba yawajumbe wa Baraza yenye kuelezea wasiwasi mkuu ulioivaa jamii ya kimataifa juu ya kuharibika kwa hali ya kisiasa, usalama na vile vile mazingira ya kiutu nchini Usomali.

Demokrasia inaanza kushika mizizi DRC, asema KM Ban

Katika ripoti ya UM iliowasilishwa karibuni kusailia hali katika JKK (DRC) KM Ban Ki-moon alithibitisha kwamba usalama wa taifa uliathiriwa nchini na haki za binadamu ziliharamishwa kwa sababu ya kuzuka migogoro miwili; kwanza, uhasama uliochipuka, baada ya kufanyika uchaguzi, baina ya serikali na wafuasi wa Makamu Raisi wa zamani, Jean-Pierre Bemba na, pili, mikwaruzuano ilioselelea kieneo kati ya Jeshi la Taifa na wanajeshi waasi, ambao huongozwa na Jenerali aliyetoroka jeshi Laurent Nkunda.

Juhudi za kuleta amani kaskazini Uganda/Mjadala wa kupanua wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama

Baada ya karibu miongo miwili ya mateso na vita, wananchi wa kaskazini wa Uganda wameanza kupumua na kuishi maisha ya kawaida, kutokana na juhudi za kurudisha tena usalama na amani kieneo.

Juhudi za kuleta amani kaskazini Uganda/Mjadala wa kupanua wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama

Baada ya karibu miongo miwili ya mateso na vita, wananchi wa kaskazini wa Uganda wameanza kupumua na kuishi maisha ya kawaida, kutokana na juhudi za kurudisha tena usalama na amani kieneo.

‘Enzi ya matumaini’ kwa Sierra Leone anasema Ban Ki-moon kwa kuapishwa rais mpya.

Akimpongeza rais Ernest Bai Koroma kwa kula kiapu kama rais mpya wa Sierra Leone, katibu mkuu wa UM Ban Ki-moon alitangaza kwamba Sierra Leone inaingia katika enzi ya matumaini, lakini alionya kwamba mptio kuelekea amani, utulivu na ukuwaji wa uchumi wa kudumu baada ya miaka mingi ya vita itakua ngumu.

Ban Ki-moon anasihi 'sheria za kulinda watoto ziheshimiwe'

KM Ban Ki-moon ameripotiwa akiunga mkono zile juhudi zinazoendelea za Serikali ya Chad katika kutafuta suluhu ya kuridhisha juu ya ule mgogoro wa karibuni, viliotukia nchini humo ambapo shirika lisio la kiserekali la Ufaransa, Arche de Zoé lilipojaribu kuwatorosha watoto 103 kutoka Chad bila ya idhini ya wazee wao.

Hapa na pale

KM Ban Ki-moon ameihimiza Pakistan kuwatoa vizuizini wafungwa wote wapinzani waliotiwa ndani majuzi, akiwemo pia Asma Jahangir, mtaalamu anayehusika na haki za uhuru wa kidini na kiitikadi; na pia KM alipendekeza kwa wenye madaraka Pakistan kuchukua hatua za haraka kurudisha tena utawala halali wa kidemokrasia nchini.