Malengo ya Maendeleo Endelevu

India kuwa mwenyeji wa siku ya mazingira duniani 2018: UNEP

Leo waziri waziri wa mazingira, misitu na mabadiliko ya tabia nchi wa India, Dr. Harsh Vardhan, na Katibu mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa mazingira UNEP Erik Solheim, kwa pamoja mjini Delhi India,  wameitangaza India kuwa mwenyeji wa siku ya mazingira duniani kimataifa kwa mwaka huu.

FAO yazindua mwongozo wa kupambana na viwavi jeshi Afrika

Leo shirika la chakula na kilimo FAO limezundua mwongozo wa kina wa kudhibiti wadudu hatari  kwa mahidi, viwavi jeshi katika barani Afrika. 

Shirika la skauti na UNEP waafikiana kutoa elimu na kulinda mazingira

Shirika la muungano wa skauti duniani (WOSM) na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa mazingira UNEP leo wamedumisha ushirikiano wao kuhusu masuala ya mazingira kwa kutambua changamoto kubwa zinazoikabili dunia hivi sasa na umuhimu wa mchango wa vijana katika kujenga dunia endelevu kandoni mwa jukwaa la kimataifa la miji mjini Kuala Lumpur.

Wanawake wa mashinani ni waleta mabadiliko

Baada ya kuonekana kuwa wananufaika na walengwa kwa muda mrefu, wanawake sasa ni vinara wa kuleta mabadiliko katika miji endelevu, na hii imewezekana baada ya wenyewe kuwa mstari wa mbele kutambua shida zinazowakabili na majibu sahihi ya matatizo yao.

Tuna mikakati thabiti ya kutimiza SDGs:Kenya

Serikali ya Kenya imesema ina mipango thabiti ya kutimiza agenda ya maendeleo endelevu au SDG's ifikapo mwaka 2030, ikiwemo mikakati ya miaka mitano iliyojiwekea kuanzia sasa hadi mwaka 2022. John Kibego na maelezo zaidi.