Malengo ya Maendeleo Endelevu

Unaweza kubeba mkoba uliotengenezwa kwa ngozi ya samaki?

Nchini Kenya harakati za shirika la chakula na kilimo duniani, FAO la kuchaguzi matumizi bora ya rasilimali za bahari zimezaa matunda baada ya wajasiriamali kuitikia wito na kutumia ngozi ya samaki aina ya sangara kutengeneza bidhaa za kibiashara. 

Sasa popote ulipo unaweza kuona msitu wowote duniani bila gharama

Kitendo cha mtu kuweza kuona misitu au miti sasa inatarajiwa kuwa rahisi zaidi kutokana na teknolojia mpya ya kisasa iliyobuniwa kwa ushirikiano kati ya shirika la anga za juu la Marekani, NASA na shirika la chakula na kilimo duniani, FAO na wadau wengine wakiwemo Google.

Ndoa za utotoni bado zawanyemelea watoto wa kike Malawi- Ripoti

Nchini Malawi, licha ya mafanikio  yaliyopatikana katika kupunguza ndoa za utotoni kwa watoto wa kike, bado mtoto mmoja kati ya wanne anaozwa kabla ya kutimiza umri wa miaka 18.

Ujuzi wa kutumia TEHAMA bado unasuasua- Ripoti ITU

Wakati idadi ya watu wanaotumia intaneti ikiongezeka duniani watu walio na ujuzi wa teknolojia, habari na mawasiliano, TEHAMA wanahitajika ili kuweza kuunganisha watu popote pale kwa mujibu wa ripoti ya muungano wa kimataifa wa mawasiliano,ITU.

Milima ni muhimu tuilinde kwa faida ya sasa na vizazi vijavyo

Leo ni siku ya milima duniani ambapo Umoja wa Mataifa unapigia chepuo  maeneo hayo kwa kaulimbinu milima ni muhimu.

Somalia yatangaza vita dhidi ya ufisadi

Serikali ya Somalia imetangaza  mikakati ya kuimarisha vita dhidi ya ufisadi na kuimarisha uwazi ili kujenga  taasisi ambazo zinawajibika.

Mauritius yaibuka kidedea biashara mtandaoni Afrika.

Mauritius imechukua nafasi ya juu kwa nchi za bara Afrika zenye utayari wa kufanya biashara kwa njia ya mitandao.

Watu zaidi ya 500 wakamatwa Papua Indonesia, UN yatiwa hofu

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa mataifa imesema inatiwa hofu na hatua ya kukamatwa watu zaidi ya 500 waliokuwa wakiandamana kwa amani kuadhimisha siku ya taifa Papua Magharibi.

Asilimia 51 watu duniani watatumia intaneti ifikapo mwisho wa 2018-ITU

Asilimia 51.2 ya watu wote duniani sawa na watu bilioni 3.9 watakuwa wanatumia mtandao wa intaneti ifikapo mwishoni mwa mwaka huu wa 2018, kwa mujibu wa makadirio mapya yaliyotolewa leo na ITU ambalo ni shirika la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya habari na teknolojia ya mawasiliano au ICTs.

Raia zaidi ya 100 wanauawa au kujeruhiwa Yemen kila wiki:UNHCR

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limetoa wito wa ulinzi zaidi kwa raia na miundombinu yao nchini Yemen baada ya tathimini yake kubaini kwamba takriban raia 1500 walijeruhiwa na wengine kuuawa kati ya Agosti na Oktoba mwaka huu, hii ikimaanisha kwamba wastani wa raia 123 waliuawa au kujeruhiwa kila wiki katika muda huo wa miezi miwili.