Malengo ya Maendeleo Endelevu

Teknolojia yaweza kuwa mkombozi wa maendeleo duniani:FOSS4G 2018

Mkutano wa kimataifa wa kutumia ubunifu wa ramani mtandaoni kufuatia picha zilizopigwa na ndege zisizokuwa na rubani au drones, unaendelea hivi sasa jijini Dar es Salaam nchini Tanzania, ukiwaleta pamoja wadau zaidi ya1000 kutoka nchi mbalimbali duniani.  

Vijana wasanii wana silaha ya kuchagiza haki za binadamu katika jamii zao

Sanaa ni moja ya mbinu inayoweza kutumika katika jamii kufikisha ujumbe na kuchagiza kuhusu malengo ya maendeleo endelevu ikiwemo lengo la haki za binadamu, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa. John Kibego na tarifa kamili

Wakimbizi milioni nne wakosa elimu; UNHCR

Ripoti mpya ya shirika la Umoja wa Mtaifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, imesema  watoto wakimbizi zaidi ya milioni nne hawapati fursa ya kuhudhuria shule wakati huu ampapo idadi ya wanaokimbia vita na majanga mengine inaongezeka duniani kote.

Mafunzo ya lugha ya Kingereza yawa mkombozi kwa wanawake Abyei:IOM

Mafunzo  ya lugha ya Kingereza yanayotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji,  IOM kwenye jimbo la Abyei yamekuwa mkombozi mkubwa kwa wanawake hasa katika kujikimu kiuchumi. 

Ubia wa UN na NGOs ni muhimu ili kufanikisha SDGs - Byanyima

Mkutano wa 67 kati ya asasi za kiraia, NGOs, na Idara ya mawasiliano ya kimataifa ya Umoja wa Mataifa unaanza leo kwenye  makao makuu ya Umoja huo jijini New York Marekani ukilenga kusaka mbinu bora za pande mbili hizo kushirikiana ili kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs.

Ujumuishwaji wa jamii ya asili katika SDGs ndio siri ya mafanikio : Dk Laltaika

Ili kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs, serikali na asasi za kiraia duniani kote zinahimizwa kuzijumuhisha na pia kuzishirikisha jamii za watu wa asili katika mikakati ya kitaifa na kimataifa ya ajenda hiyo ya 2030

Uwekezaji wa dola 1 kwa wafugaji Kenya wapatia kila kaya ya wafugaji dola 3.5- FAO

Mradi wa pamoja wa shirika la chakula na kilimo FAO na serikali ya Kenya wa kutoa onyo mapema kuhusu majanga umesaidia wafugaji kukabiliana na ukame na kuepusha njaa na vifo.

ILO yasaidia stadi za kazi kwa magenge ya zamani ya uhalifu Madagasacar

Shirika la kazi duniani, ILO nchini Madagascar linaendesha mafunzo ya stadi za kazi kwa vijana wasio na ajira hususan wale waliokuwa wafuasi wa magenge  ya uhalifu ili hatimaye waweze kuajiriwa au kujiajiri.

Nina Imani na uwezo walio nao vijana:Guiterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema ana imani na uwezo walionao vijana katika kuleta mabadiliko duniani. Flora Nducha na tarifa zaidi

Uhakika wa chakula ni mtihani mkubwa kwa watu wa jamii za asili: FAO

Uhakika wa chakula umeelezwa kuwa ni changamoto kubwa kwa watu wa jamii za asili hususan wanawake ambao ndio walezi wa familia na jamii.