Malengo ya Maendeleo Endelevu

Mpango wa kusaidia Sahel wazinduliwa leo, utajiri wa ukanda huo wawekwa bayana

Umoja wa Mataifa umesema rasilimali lukuki zilizopo kwenye ukanda wa Sahel ni moja ya suluhu mujarabu ya matatizo yanayokabili eneo hilo.

Kipaji cha mwanao ni kwa ajili yake na jamii yake

Unaposaidia kuendeleza kipaji cha mwanao faida zake si kwake peke yake bali pia kwa jamii nzima. Huo ndio wito uliojitokeza katika warsha ya siku tatu iliyokutanisha wazazi, walimu na wanafunzi mkoani Pwani nchini Tanzania kwa lengo la kutambua, kuendeleza na kufaidi na vipaji vya watoto hususani yatima na wasiojiweza.

Kulemaa viungo sio kulemaa akili- Dkt. Sankok

Kuwa na ulemavu wa aina yoyote ile hakumaanishi umelemaa akili na watu wenye ulemavu wana uwezo mkubwa na mchango katika jamii kama walivyo watu wengine wasio na ulemavu amesema Dkt. kutoka jamii ya Wamasai ya Narok nchini Kenya

Wanawake ndio wanaobeba gharama kubwa ya huduma zisizo na ujira:ILO

Uwekezaji katika uchumi utokanao na sekta ya huduma unahitaji kupigwa jeki mara mbili ili kuepuka janga la kimataifa linalonyemelea katika sekta hiyo, imesema ripoti mpya ya shirika la kazi duniani ILO iliyotolewa leo

Saudi Arabia waachilieni wanawake mliokamata- Wataalamu

Wataalam wa masuala ya haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa  wameitaka serikali ya Saudi Arabia iwaachilie huru mara moja  wanawake wanaharakati waliowekwa ndani katika msako uliofanyika nchini humo hivi karibuni, wakati huu ambapo taifa hilo limeondoa marufuku ya wanawake kuendesha magari.

 

Vipepeo vyawapaisha kiuchumi wanakijiji wa Amani Tanga.

Mradi wa vipepeo katika hifadhi ya taifa  ya  Amani mkoani Tanga nchini Tanzania umekuwa mkombozi mkubwa  kiuchumi hususani kwa wanawake wa vijijini.

Tangu Juni 6 hakuna visa vipya vya Ebola DRC:WHO

Shirika la afya ulimwenguni WHO,  limesema limefanikikiwa kwa kiasi kikubwa  kuzuia mambukizi mapya na  kusambaa kwa ugonjwa wa ebola katika mkoa wa Mbandaka, nchini jamhuri ya kidemokrasia ya Congo DRC.

Matumizi ya dawa za maumivu bila kibali yasababisha vifo vya watu wengi duniani- UNODC.

Ripoti ya  mwaka 2018 ya ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kupambana na madawa ya kulevya na uhalifu, UNODC, imebaini kuwa matumizi ya dawa za  maumivu bila kibali cha madaktari yamesababisha vifo vya zaidi ya asilimia 76 ya watumiaji duniani kote.

Usafirishaji bora baharini hutegemea ustawi wa mabaharia-IMO

Ustawi  na ufanisi wa shughuli za baharini unategemea  afya  imara na mazingira salama  na endelevu  kwa mabaharia.

UNCTAD na Ali Baba washirikiana kukwamua vijana

Maendeleo ya teknolojia yanazidi kuleta nuru duniani ambapo Umoja wa Mataifa nao unatumia fursa ya kupitia wadau wake ili kuona maendeleo hayo yananufaisha watu wote ikiwemo vijana hususan wale wa pembezoni.