Malengo ya Maendeleo Endelevu

WHO na WMO kudhibiti athari za kiafya na hali ya hewa

Mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa yamekubaliana kuanzisha  mkakati maalum wa pamoja utakaosaidia kudhibiti athari za kiafya zinazosababishwa na mazingira duni.

Acheni kutumia viuavijasumu kukuza mifugo-FAO

Umoja wa Mataifa umetaka wafugaji kuacha mara moja tabia ya kutumia viuavijasumu kukuza mifugo yao pamoja na kuku, ukisema kuwa dawa hizo ni kwa ajili ya matibabu na si vinginevyo.

Tuwekeze katika elimu na ajira ili tuokoe vijana dhidi ya itikadi kali :Lajčák

Leo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa kumefanyika mdahalo wa vijana ulioandaliwa na rais wa mkutano wa 72 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwa lengo la kuwahamasisha vijana katika masuala ya elimu, ajira na pia mazungumzo kuhusu athari za kutumbukia kwenye itikadi kali

Je wanavijiji watamudu nishati mbadala ili kulinda misitu Tanzania?

Katika jitihada za pamoja za Umoja wa Mataifa  na serikali duniani kuhakikisha misitu inalindwa ili kudhibiti mabadiliko ya tabianchi, Tanzania imejiwekea mkakati kabambe wa  miaka 5 kwenda sanjari na lengo hilo.

Watoto zaidi ya milioni nchini Mali hawasomi

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF, Henrietta Fore anazuru Mali ambako miaka sita baada ya kuanza mgogoro wa kaskazini mwa nchi hiyo ghasia zinazidi kuongezeka huku watoto nao wazidi kunyimwa haki zao kama vile chakula, elimu na kuishi.

Uhamiaji uwe ajenda ya kisiasa barani Afrika

Mkutano wa siku mbili kuhusu uhamiaji barani Afrika umekunja jamvi huko Geneva, Uswisi ambapo washiriki wametaka viongozi wa bara hilo wahamasishwe ili uhamiaji iwe ajenda ya kisiasa kwa nchi zao.

Vita dhidi ya ufisadi ni chachu kwa SDGs

Rushwa ni adui wa haki, ni kauli ambayo hii leo imepatiwa mkazo wakati wa maadhimisho ya miaka 15 ya mkataba wa kimataifa wa kupambana na rushwa duniani.

Korea Kusini badilisha sera ya makazi- UN

Korea Kusini imeshauriwa  kubadili sera yake kuhusu  makazi na wasio na makazi ili kuweza kufikia viwango vinavyohitajika sasa vya haki za binadamu.

Mkakati mpya wa WHO kuokoa watu milioni 29 ifikapo 2023

Wajumbe wa mkutano wa Baraza Kuu la shirika la afya ulimwenguni, WHO wameridhia mpango mpya wa mkakati wa  miaka mitano wenye lengo la kusaidia kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu SDGs.

Kaunti ya Meru yaonyesha mfano kusaidia vijana

Kaunti ya Meru nchini Kenya imezindua mpango wa miaka 5 wenye lengo la kuleta upya matumaini kwa vijana waliopoteza matumaini ya kujipatia kipato baada ya Muungano wa Ulaya kupiga marufuku bidhaa ya miraa yenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 6.