Amani na Usalama

MONUSCO na harakati za kudhibiti kuenea kwa COVID-19 nchini DRC

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako idadi ya wagonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19 ambao wamethibitishwa hadi leo hii ni 109 huku 8 (wanane) kati yao tayari wamefariki dunia, Umoja wa Mataifa umechukua hatua kuunga mkono hatua za serikali za kudhibiti kusambaa zaidi kwa virusi hivyo miongoni mwa wananchi wanaowahudumia na wafanyakazi wake.

Vifo kutokana na COVID-19 duniani sasa 21,031, OCHA yahofia kwenye mizozo na majanga

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu, OCHA leo imezungumzia hofu yake jinsi majanga na mizozo inavyoendelea kuwa kikwazo katika kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa virusi vya Corona, COVID-19 huko Syria, Libya na Afghanistan huku ikipongeza hatua zilizochukuliwa na Sudan katika kukabiliana na kuenea kwa ugonjwa huo.

Pande kinzani Sudan wekeni silaha chini tokomezeni COVID-19

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika, AU, huko Darfur, Sudan, Jeremiah Mamabolo amekazia kauli ya Katibu Mkuu wa umoja huo ya kutaka sitisho la mapigano kwenye maeneo ya mizozo wakati huu ambapo virusi vya Corona, COVID-19, vimeshasambaa katika mataifa 194.

Yemen sitisheni uhasama mjikite na COVID-19:Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametoa wito kwa pande kinzani katika mzozo wa Yemen kusitisha uhasama mara moja na kujikita katika majadiliano ya suluhu ya kisiasa huku wakifanya kila wawezalo kukabiliana na virusi vya Corona, COVID-19.

UN yachukua hatua kusaidia maandalizi ya vita dhidi ya COVID-19 Sudan Kusini

Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini umetangaza hatua mpya katika kusaidia juhudi zinazoongozwa na serikali ya Sudan kusini katika kuzuia na kujiandaa na mlipuko wa virusi vya Corona, COVID-19.

Hukumu dhidi ya viongozi wa vyama vya upinzani Tanzania inaonesha kuendelea kutetereka kwa uhuru wa raia-UN

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu OHCHR kupitia taarifa yake iliyoitoa hii leo jumanne Machi, 17, 2020 mjini Geneva Uswisi na Addis Ababa Ethiopia imeeleza kuwa hukumu ya hivi karibuni dhidi ya viongozi wa kisiasa nchini Tanzania ni ushahidi tosha wa kutetereka kwa uhuru wa raia nchini humo.

Mlinda amani wa UN kutoka Burundi auawa CAR, Guterres azungumza

Umoja wa Mataifa umeripoti hii leo ya kwamba mlinda amani wake kutoka Burundi ameuwa kwenye mji wa Grimari ulioko katikati mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR.
 

Ingawa nina miaka 11 najihisi nina miaka 100: mtoto Naamat

Wakati vita vya Syria vikiwa vimetinga miaka tisa sasa maelfu ya watoto maisha yao yanaendelea kuwa njiapanda wengi wakiwa wamepoteza wazazi na kila kitu na wengine kulazimika kukua kuliko umri wao.

Sijawahi kushuhudia amani maishani mwangu: Mkimbizi Rotto

Tangu nizaliwe sijawahi kushuhudia amani, hiyo ni kauli ya mkimbizi wa ndani wa Sudan Kusini John Rotto mwenye miaka 65, aliyezaliwa na kukulia kwenye vita.kulikoni? 

Kwa watoto wa Syria miaka 9 ya mzozo ni sawa na kuwepo jehanam- Unicef

Takribani watoto milioni 4.8 wamezaliwa nchini Syri tangu mapigano yaanze nchini humo miaka 9 iliyopita, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF.