Amani na Usalama

Nchi 170 zaidhinisha ombi la usitishaji uhasama wakati wa janga la COVID-19: UN

Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, nchi waangalizi na wengineo wametuma ujumbe mzito wa kisiasa wiki hii kwa kutangaza kwamba sahihi 170 sasa zimeidhinisha wito wa Umoja wa Mataifa wa kunyamazisha silaha na kusimama Pamoja dhidi ya tishio la kimataifa la janga la virusi vya corona au CIVID-19.

Chonde chonde Israel acheni upanuzi wa makazi ya Walowezi Ukingo wa Magharibi:UN

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akizungumza kwa njia ya video kwenye Baraza la Usalama hii leo ametoa wito kwa Israel na kuisihi kutotekeleza mipango yake ya upanuzi wa makazi ya walowezi kwenye Ukingo wa Magharibi.

Mlinda amani wa Umoja wa Mataifa auawa Kivu Kaskazini, UN yalaani vikali

Mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa na mkuu wa mpango wa Umoja huo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo MONUSCO, amelaani vikali mauaji ya mlinda amani wa Umoja wa Mataifa yaliyofanyika usiku wa kuamkia leo.

Baraza la haki za binadamu lapitisha azimio kutaka ubaguzi wa rangi dhidi ya watu wa asili ya Afrika ukomeshwe

Kamishina Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet kuongoza juhudi za kushughulikia mfumo wa ubaguzi wa rangi dhidi ya watu wenye asili ya Afrika unaofanywa na vyombo vya dola vya ulinzi na usalama.

Ulinzi wa amani na michezo wadhihirika huko Mavivi, DRC

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, walinda amani kutoka Tanzania wanaohudumu katika kikosi cha 7 cha nchi hiyo, TANZBATT 7, cha kujibu mashambulizi, FIB, cha ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, MONUSCO wamepanua wigo wa ukarimu wao kwa watoto na vijana wa eneo la Mavivi, mjini Beni jimboni Kivu Kaskazini.

Mtoto 1 kati ya 2 duniani anapitia ukatili na nchi zimeshindwa kuuzuia:UN

Ripoti mpya iliyotolewa leo na Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya kimataifa ya kuzuia ukatili dhidi ya watoto imeonya kwamba nchi zimeshindwa kuzuia ukatili huo dhidi ya watoto na kutoa wito kwa nchi kuchukua hatua kuzuia athari kubwa zaidi.

Shehena nyingine ya vifaa vya uchaguzi yawasili CAR

Nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR,  shehena ya tatu ya vifaa vya uchaguzi imewasili katika mji mkuu wa nchi hiyo Bangui. Vifaa hivyo vimetolewa na Umoja wa Mataifa na wadau wake ukiwemo Muungano wa Ulaya, EU,  na ni kwa ajili ya uchaguzi wa Rais na wabunge uliopangwa kufanyika nchini humo mwezi Desemba mwaka huu.

Pamoja na kulinda amani, TANZBATT 7 yatoa msaada hospitali kuu Beni

Hospitali kuu ya Beni jimboni Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC imeshukuru msaada wa dawa kutoka kikosi cha Tanzania kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini  humo, MONUSCO  ikisema kuwa msaada huo umekuja wakati muafaka. 

UN yalaani vikali shambulio dhidi ya raia huko Monguno Nigeria lililoua watu 40

Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Nigeria Edward Kallon amelaani vikali shambulio la kikatili lililofanywa na makundi yenye silaha kwenye eneo la Monguno Nganzai nchini Nigeria siku ya Jumapili.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa atuma salamu za pole kwa waathirika wa shambulizi la Jumamosi nchini Mali

Katibu Mkuu wa Umoja wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wake hii leo Jumapili na mjini New York Marekani, amelaani vikali shambulizi lililofanyika jana Jumamosi dhidi ya msafara wa mpango wa Umoja wa Mataifa wa kuweka utulivu nchini Mali, MINUSMA uliokuwa ukisafiri kati ya Tessalit na Gao, tukio ambalo liliwaua walinda amani wawili wa Umoja wa Mataifa raia wa Misri.