Amani na Usalama

Matatizo ya kiutu kukithiri katika CAR

Shirika la Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limeripoti kwamba hali mbaya ya kiutu inaendelea kusambaa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) ambapo mamia elfu ya raia waliong’olewa makwao, kwa sababu ya hali ya vita na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe, wanahitajia kufadhiliwa kidharura misaada ya chakula kunusuru maisha. Hali hii sasa hivi imechafuliwa zaidi kutokana na vurugu liliofumka na kufurika kutokea eneo jirani la Darfur, Sudan.

UM unakumbuka mauaji ya Rwanda

Tarehe 09 Aprili, iliadhimishwa na UM kuwa ni siku ya kuukumbuka umma wa Rwanda ulioteswa na kuuliwa kikatili miaka 13 iliopita. Kwa mujibu wa ripoti za kimataifa, makundi ya majambazi na maharamia, waliokuwa wamechukua mapanga na mabunduki, waliamua kumaliza mauaji yao ya kikatili yalioangamiza watu 800,000 ziada kutoka sehemu zote za Rwanda.

Jumuiya ya kimataifa yasikitika na kulaani mashambulio ya mabomu Algeria na Iraq

Maofisa wa UM wa vyeo vya juu, wakijumuika na KM Ban Ki-moon walishtumu na kulaani vikali mashambulio maututi yaliotukia majuzi kwenye Bunge la Iraq, Baghdad, ambapo Wabunge kadha walifariki na wingi wengineo kujeruhiwa.

Hali mbaya kusini-mashariki ya Chad imekiuka makadirio ya UNHCR

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) imeripoti ya kuwa hali kusini-mashariki ya Chad imeharibika sana na imekiuka makadirio, mazingira ambayo yalijiri baada ya kufanyika mashambulio ya kikatili, na makundi yenye silaha, dhidi ya wanavijiji, mnamo mwisho wa mwezi Machi.

Mapigano makali Usomali kuzusha msiba mkuu wa kiutu nchini: OCHA

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imeripoti kwamba hali ya kijamii, kwa ujumla, katika Usomali, ni mbaya sana kwa sasa, kutokana na mapigano makali yalioshtadi karibuni, vurugu ambalo aina yake haijawahi kushuhudiwa tangu 1991.

Meli iliokodiwa na WFP na kutekwa nyara Usomali imeachiwa huru

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limepongeza kuachiwa huru kwa ile meli ya MV Rozen, ambayo iliikodi siku za nyuma kupeleka chakula Usomali. Meli hiyo ilitekwa nyara na maharamia kwenye mwambao wa eneo la Puntland mnamo Februari 25 mwaka huu.

MONUC ilimsaidia kiongozi wa upinzani DRC kupata kibali cha kwenda Ulaya kwa matibabu

Ripoti za UM zimethibitisha kuwa Shirika linalohusika na Operesheni za Ulinzi wa Amani katika JKK (MONUC) lilishiriki kwenye mazungumzo na wenye madaraka nchini DRC ya kumpatia Seneta Jean-Pierre Bemba ruhusa ya kufanya safari ya kwenda Ulaya kwa matibabu.

Hapa na pale

WHO imepongeza uamuzi wa karibuni wa kampuni ya madawa ya Maabara ya Abbott (Abbott Laboratories) wenye dhamira ya kupunguza bei ya zile dawa za kurefusha maisha zinazojulikana kama LPV/R, ambazo huuzwa kwenye soko la kimataifa kwa kutumia jina la Kaletra/Aluvia, na hupewa wagonjwa wenye VVU na UKIMWI.~

Hapa na pale

Antonio Guterres, Kamishna Mkuu was Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR, alipokuwa ziarani Mashariki ya Kati wiki hii, aliahidi kuwa atapeleka Iraq maofisa zaidi wa shirika lake kuwasaidia kihali wale WaIraki karibu milioni 4 waliong’olewa makwao kutokana na vurugu lilioshtadi nchini mwao.~

KM na UNMIS walaani mauaji ya wanajeshi wa AMIS katika Darfur

KM Ban Ki-moon amearifu kuhuzunishwa na mauaji ya kihorera ya wanajeshi watano wa vikosi vya ulinzi wa amani vya Umoja wa Afrika (AMIS) yaliyofanyika Ijumapili iliopita katika eneo la Um Baru, kilomita 220 kutoka El Fasher, mji mkuu wa jimbo la Darfur ya Kaskazini.