Amani na Usalama

Mapitio ya Kazi za UM 2007

Mnamo mwaka 2007 UM ulikabiliwa na matatizo kadha wa kadha yaliohitajia suluhu ya pamoja, kutoka jamii ya kimataifa, kwa UM kufanikiwa kulinda usalama na amani na kuimarisha maendeleo ya uchumi na jamii yatakayokuwa na natija kwa umma pote duniani.

Mapitio ya Kazi za UM 2007

Mnamo mwaka 2007 UM ulikabiliwa na matatizo kadha wa kadha yaliohitajia suluhu ya pamoja, kutoka jamii ya kimataifa, kwa UM kufanikiwa kulinda usalama na amani na kuimarisha maendeleo ya uchumi na jamii yatakayokuwa na natija kwa umma pote duniani.

UNMEE inakhofia usalama kuharibika mipakani Ethiopia/Eritrea

Shirika la UM juu ya Operesheni za Amani Mipakani Ethiopia na Eritrea (UNMEE) limeripoti kuwa na wasiwasi kuhusu utulivu wa mipaka kwenye Eneo la Usalama wa Muda (TSZ), baada ya kutukia mashambulio ya risasi karibuni katika Tsorena, eneo iliopo upande wa Eritrea.

Mjumbe wa KM kwa Usomali aomba mateka wa MSF waachiwe huru

Mjumbe Maalumu wa KM kwa Usomali, Ahmedou Ould-Abdallah amesema ameshtushwa na utekaji nyara wa wafanyakazi wawili wa shirika la madakatari, lisio la kiserekali la Medecins Sans Frontieres (MSF) uliojiri karibuni katika mji wa Bosasso, Puntland.

Ujambazi Chad mashariki wailiazimisha UM kupunguza misaada ya kiutu kwa umma muhitaji

Ofisi ya UM inayohusika na Misaada ya Dharura (OCHA) imeripoti kwamba majambazi bado wanaendelea kuhujumu wafanyakazi wa kimataifa wanaohudumia misaada ya kiutu katika sehemu kadha nchini Chad, hali ambayo inazorotisha zile juhudi za kuitekeleza kadhia hiyo umma muhitaji.

KM anatumai uamuzi wa kuitisha mkutano wa kusailia hali katika Kivu utawasilisha amani

UM umepongeza uamuzi uliofikiwa karibuni na Serikali ya JKK pamoja na wakazi wa majimbo ya Kivu Kusini na Kaskazini kuitisha Mkutano wa Kuzingatia masuala ya Amani, Usalama na Maendeleo katika eneo lao lenye matatizo.

UNHCR yahimiza mapigano yakomeshwe Kivu Kaskazini kunusuru raia

Antonio Gutteres, Kamishna Mkuu wa Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) ambaye alizuru Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (JKK)hivi karibuni, ametoa mwito wenye kuyanasihi makundi yote yalioshiriki kwenye uhasama na mapigano katika jimbo la Kivu Kaskazini, kusitisha mapigano haraka iwezekanavyo, hali ambayo ikikamilishwa itayawezesha mashirika ya kimataifa yanayofadhilia misaada ya kiutu kupata fursa ya kuhudumia kihali umma muhitaji ulionaswa kwenye mazingira ya mapigano.

Baraza la Usalama laongeza madaraka ya shirika la BINUB Burundi

Baraza la Usalama limepitisha azimio la kuongeza muda wa kazi za Ofisi ya UM inayosimamia ufufuaji wa shughuli za maendeleo katika Burundi (BINUB) hadi tarehe 31 Disemba 2008.

Baraza la Usalama kujadidisha vikwazo dhidi ya Liberia

Baraza la Usalama limepitisha azimio nambari 1792 ambalo limependekeza vikwazo vya silaha, na usafiri dhidi ya baadhi ya viongozi katika Liberia, viendelezwe kwa miezi 12 zaidi.

Mjumbe wa KM amependekeza diplomasiya itumiwe kukabiliana na vurugu Usomali

Ahmedou Oul-Abdallah, aliye Mjumbe Maalumu wa KM kwa Usomali aliwaambia wawakilishi wa katika Baraza la Usalama wiki hii, kwenye mkutano wa hadhara, ya kwamba wakati umeshawadia kwa wao kuandaa ramani hakika ya kidiplomasiya, ili kuisaidia Usomali kurudisha tena hali ya utulivu na amani nchini.