Wahamiaji na Wakimbizi

Tuna hofu kubwa baada ya wahamiaji 100 kufa maji Tunisia:IOM

Wahamiaji takriban 100 wamekufa maji, 68 kunusurika na wengine hawajulikani waliko baada ya boti yao kuzama mwambao wa Kerkennah-Sfax nchini Tunisia mwishoni mwa wiki.

Baada ya kuporwa utoto wao na vita, sasa maelfu ya watoto waishia ukimbizini Uganda

Wahudumu wa mashirika ya misaada ya kibinadamu nchini Uganda wakiwemo wa Umoja wa Mataifa wanakumbana na changamoto kubwa ya kuwasaidia watoto wakimbizi zaidi ya 25,000 waliotengana na wazazi ama walezi wao kutokana na vita na kusaka hifadhi wakiwa peke yao nchini humo. Mwandishi wetu wa Uganda  John Kibego ametembelea makazi ya wakimbizi ya Imvepi Wialayani Arua nchini humo ambako kuna asilimia kubwa ya watoto  na kuandaa tarifa hii.

Wasafirishaji haramu wa binadamu wameua watu 12 Libya manusura wasaidiwa na UNHCR

Watu 12 wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa baada ya wasafirishaji haramu wa binadamu nchini Libya kuwafyatulia risasi watu 200 waliokuwa wakishikilia mateka wakati walipojaribu kutoroka. 

Wakimbizi walio taabani Jordan waomba msaada usikatwe

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR linahitaji msaada wa haraka wa dola milioni 116 ili kuendeleza mpango wa kusaidia wakimbizi wa Syria wasiojiweza nchini Jordan.

UNHCR inasema fedha hizo zisipopatikana, italazimika kukata msaada wa fedha kwa wakimbizi wa Syria walioko Jordan ikiwemo walio taabani.

Rwanda yaanzisha viza maalum ya kuchochea wahamiaji wenye ujuzi

Nchi za Afrika sasa zaamka na zimeanza kujiwekea mifumo bora ya kisera ili uhamiaji uwe na matunda ndani  ya bara hilo.

Hungary tupilieni mbali mswada wa sheria zitakayowaathiri wakimbizi: UNHCR

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, limetoa wito kwa serikali ya Hungary kuachana na mswada wa sheria zinazotarajia kuwasilishwa bungeni ambazo zitabana uwezo wa mashirika yasiyo ya kiserikali NGO’s na watu binafsi kuwasaidia waomba hifadhi na wakimbizi.

IOM yasaidia kuwarejesha Ethiopia wahamiaji 100 Kutoka Yemen

Raia 101 wa Ethiopia waliokuwa wahamiaji nchini Yemen wameondoka kwa hiyari kwa msaada wa shirika la uhamiaji la Umoja wa Mataifa IOM na kurejea nyumbani kupitia bandari ya Hudaydah.

Uhamiaji uwe ajenda ya kisiasa barani Afrika

Mkutano wa siku mbili kuhusu uhamiaji barani Afrika umekunja jamvi huko Geneva, Uswisi ambapo washiriki wametaka viongozi wa bara hilo wahamasishwe ili uhamiaji iwe ajenda ya kisiasa kwa nchi zao.

Badala ya beseni la chakula, watoto DRC wabeba beseni la mchanga

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, vita na janga la kibinadamu nchini humo vimesababisha watoto kulazimika kufanya kazi ili waweze kutunza familia zao. Grace Kaneiya na ripoti kamili.

Algeria acheni kuwatimua kwa pamoja wahamiaji:UN

Umoja wa Mataifa leo umetoa wito kwa serikali ya Algeria kusitisha vitendo vya kuwafukuza kwa pamoja wahamiaji hususani kutoka Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara. Ingawa idadi kamili ya waliotimuliwa haijajulikana inaaminika ni maelfu ya wahamiaji.