Wahamiaji na Wakimbizi

Sijutii kupoteza mali zangu ilimradi familia yangu ipo salama

Baada ya kupoteza kila  kila kitu wakati wa  migogoro wa kivita nchini kwao Burundi , mwanamke mkimbizi aliyekimbilia Rwanda  anasema , hajutii mali na vitu alivyovipoteza  kwani yeye na familia yake wapo salama aliko ukimbizini.

Hatari bado ipo kwa wakimbizi takriban milioni 1 wa Rohingya: WHO

Shirika la afya ulimwenguni WHO linaendelea na juhudi za kuwalinda wakimbizi wa Rohingya karibu milioni moja nchini Bangladesh dhidi ya ugonjwa wa kipindupindu, huku leo likionya kwamba hatari bado ipo.

Makazi mbadala kwa warohingya yakamilika- UN

Mashirika ya misaada ya kibinadamu yanayotoa huduma kwenye kambi za wakimbizi wa Rohingya nchini Bangladesh , leo yamekamilisha maandalizi ya eneo la kwanza jipya kwa ajili ya kuhamishia familia za wakimbizi walio katika hatari ya maporomoko yatakayosababishwa na pepo za monsuni. 

Lindeni wahamiaji-IOM

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wahamiaji IOM lina wasiwasi kutokana na hali mbaya ya wahamiaji  nchini  Yemen.

 

Ukarimu wa waganda wavutia wakimbizi

Uganda ni miongoni mwa mataifa ambayo  yanayoendelea kupokea wakimbizi kutoka nchi jirani ya jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC . Wakimbizi hao wanatoka maeneo ya mashariki mwa nchi hiyo na sasa wamefika ugenini Uganda na wanajiona wako nyumbani kutokana na ukarimu wa wenyeji. 

Machafuko yafurusha zaidi ya 11,00, na vijiji vyachomwa Darfur

Takriban watu 11, 500 wamelazimika kufungasha virago na kukimbia nyumba zao kufuatia machafuko kwenye mji wa Rokero eneo la Jebel Marra jimbo la Darfur nchini Sudan.

Wapata kiwewe baharini, UNHCR yaelekeza usaidizi

Nchini Libya, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi,  UNHCR limeanza awamu ya pili ya kusaidia wakimbizi na wahamiaji waliookolewa mjini Tripoli baada ya kukabiliwa na hali mbaya baharini.

Mkimbizi afariki dunia baada ya mapigano kambini Kiziba

Umoja wa Mataifa umetaka mamlaka za Rwanda na wakimbizi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC waliosaka hifadhi nchini humo wajizuie kufuatia mapigano ya wiki hii yaliyosababisha kifo cha mkimbizi mmoja.

Ingawa umri wangu ni miaka 17 tu lazima niwalee wadogo zangu.

Baada ya kuuliwa kwa wazazi wake na watu wenye silaha msichana mwenye umri wa miaka 17 alichukuwa jukumu la kuwalewa wadogo za watatu kutoka Myanmar hadi Kutupalong nchini Bangladesh

Warohingya wajiandaa kabla ya hatari ya monsuni

Nchini Bangladesh shirika la mpango wa chakula duniani, WFP linashirikiana na warohingya waliosaka hifadhi humo katika kuandaa vema makazi na uhifadhi wa chakula wakati huu ambapo msimu wa pepo za monsuni unabisha hodi.