Wahamiaji na Wakimbizi

Ghasia mpya jimboni Ituri DRC zaweka watoto katika hali mbaya zaidi- UNICEF

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, limesema mapigano yaliyoanza tena hivi karibuni katika jimbo la Ituri nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, yanazidi kuhatarisha hatma ya watoto sambamba na ripoti za ukiukwaji wa haki za wanawake.
 

Kuzama kwa meli ya Venezuela hivi karibuni, kunasisitiza umuhimu wa kuwa na njia mpya: IOM na UNHCR 

Shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji, IOM na lile la kuhudumia wakimbizi, UNHCR kupitia taarifa ya pamoja iliyotolewa mjini Geneva, Uswisi, wamesikitishwa na vifo vya watu wawili wakati boti ilipozama katika baharí Venezuela Alhamisi ya Aprili 22.

Jamii ya kimataifa msiisahau DRC, yenyewe imejitoa vya kutosha- Grandi

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR Filippo Grandi ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuimarisha msaada wake na mshikamano na wananchi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, taifa ambalo licha ya kuwa na idadi kubwa ya wakimbizi wa ndani barani Afrika, bado limekuwa na ukarimu wa kuhifadhi nusu milioni ya watu wanaokimbia mizozo katika maeneo mengine barani humo.
 

Watu 130 wafa maji Libya baada ya boti kuzama:IOM 

Boti iliyozama Pwani ya Libya imeripotiwa kukatili maisha ya watu 130, licha ya kuomba msaada wa dharura wa uokozi limesema shirika la uhamiaji la Umoja wa Mataifa IOM. 

Zaidi ya watu milioni 1 wametawanywa katika maeneo 178 kwenye jimbo la Tigray

Zaidi ya watu milioni 1 wametawanywa katika maeneo 178 kwenye jimbo la Tigray kaskazini mwa Ethiopia na majimbo ya jirani ya Afar na Amhara kwa mujibu kwa takwimu zilizotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la wahamiaji IOM.

Takribani watu 4,000 zaidi wakimbia Cabo Delgado, fedha za dharura zatolewa 

Takribani watu 4,000 wamekimbia huko Palma, kaskazini mwa Msumbiji katika wiki iliyopita, wakiongeza idadi ya wakimbizi kufikia karibia 25,000 kwa mujibu wa takwimu ziliyokusanywa na shirika la uhamiaji la Umoja wa Mataifa, IOM, ambalo wiki hii limechangia dola milioni 1.2, imeeleza taarifa ya shirika hilo iliyotolew mjini Pemba nchini Msumbiji.

Fahamu kuhusu Alaa, mkimbizi ambaye ni mfano wa nguvu katika hali ya changamoto za maisha

Kutana na Alaa, mkimbizi kutoka Syria ambaye amemudu kuwahamasisha wanawake wenzake kutoka Syria na wenyeji wake Lebanon kutumia michezo na mazoezi ya mwili ili kujenga  kujiamini na pia kujenga  jamii hata wakati wa janga la COVID-19.

Kutana na Khamisa mkimbizi anayeisaidia familia yake kupata chakula

Jimbo la White ni nyumbani mwa idadi kubwa ya wakimbizi kutoka Sudan Kusini. Katika nusu ya kwanza ya mwaka wa 2019 Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa WFP liliwasaidia wakimbiizi 387,000 kote nchini Sudan huku sehemu kubwa ya mchango wa chakula ukitoka shirike la Marekania la USAID. Nusu ya wakimbizi hao ni wanawake. 

Mapigano mapya yawafungisha virago watu 2,000 CAR na kuingia Chad:UNHCR 

Mapigano kati ya vikosi vya serikali na vikundi vya waasi kaskazini mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) yaliyozuka wiki iliyopita yamelazimisha zaidi ya raia zaidi ya 2,000 kuvuka mpaka na kutafuta hifadhi katika nchi jirani ya Chad, limesema shirika la Umoja wa Mastaifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR. 

Hakuna dalili za kumalizika mzozo Tigray yaonya UNICEF

Ripoti za kusikitisha zimeendelea kujitokeza za kusambaa kwa  unyanyasaji mkubwa wa raia katika eneo la Tigray nchini Ethiopia, karibu miezi sita tangu mzozo ulipozuka, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF.