Kufuatia kitendo cha baadhi ya wasafirishaji haramu wa binadamu huko Afrika Magharibi, kudaiwa kutumia nguvu za giza au JUJU kama tishio kwa wale wanaosafirishwa, shirika la Uhamiaji la Umoja wa Mataifa, IOM limekutana na msemaji wa chifu mmoja ambaye amechukua hatua kuondokana na fikra hizo potofu.