Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, Filipo Grandi akiwa ziarani nchini Tanzania amesema Tanzania kwa muda mrefu imekuwa ni karimu hususan kwa wakimbizi ambao wanakimbia machafuko na rais wake John Magufuli amerejelea kuwa ukarimu huo hautafika mwisho.