Wahamiaji na Wakimbizi

Guterres azindua ajenda ya hatua kukabili ukimbizi wa ndani

Dunia yetu inakabiliwa na janga la ukmbizi wa ndani! Ndivyo alivyoanza ujumbe wake Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ujumbe ambao ametoa leo kwa njia ya video kuzindua ajenda yake ya hatua dhidi ya ukimbizi wa ndani.

Ningalikataliwa kuingia Uganda, ningaliuawa – Mkimbizi kutoka DRC

Tarehe 20 mwezi huu wa Juni ilikuwa ni siku ya wakimbizi duniani ambapo Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa ilipata fursa ya kuzungumza na wakimbizi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC walioko nchini Uganda.

Idadi ya wasaka hifadhi nchi ya tatu kuongezeka 2023

Zaidi ya wakimbizi milioni 2 mwaka ujao WA 2023 watahitaji kuhamishiwa nchi ya tatu ikiwa ni ongezeko kwa asilimia 36 ikilinganishwa na mahitaji ya mwaka huu ambayo ni wakimbizi milioni 1.5 pekee, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR kupitia tathmini ya makadirio ya kuhamia nchi ya tatu kwa mwaka 2022.

Côte d'Ivoire yakaribisha familia zinazorejea kutoka ukimbizini

Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, Filippo Grandi, ameadhimisha Siku ya Wakimbizi Duniani nchini Côte d'Ivoire, pamoja na wakimbizi wa zamani ambao wamerejea nyumbani kabla ya kumalizika rasmi kwa hadhi ya ukimbizi kwa raia hao baadaye mwezi huu. 

Wakimbizi tukikirimiwa tunarejesha fadhila kwa jamii:Bahati, Micheline na Agnes

Kutana na wakimbizi Bahati Hategekimana kutoka Rwanda, Micheline Muhima kutoka Uganda na Agnes Mude kutoka Sudan Kusini ambao wote walikuwa wakiishi kwenye kambi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya, lakini sasa kupitia mradi wa majaribio wa kuthamini mchango wa wakimbizi EMPP, unaoendeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, mjini Pictou na serikali ya Canada watatu hao si wakimbizi tena bali ni wafanyakazi wa huduma ya jamii kwenye kituo cha Glen Haven Manor kilichopo jimboni Nova Scotia nchini Canada. 

Haki ya kutafuta hifadhi ni haki ya msingi ya kibinadamu: Guterres

Wakati duniani inaadhimisha siku ya wakimbizi duniani hii leo kwa kuwa na idadi kubwa kabisa ya wakimbizi kuwahi kurekodiwa, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres anasema siku hii itumike kutafakari juu ya ujasiri wa wale wanaokimbia vita, vurugu na mateso pamoja na kutambua huruma ya wale wanaowakaribisha wakimbizi hao. 

Ni uamuzi mchungu kuamua mkimbizi yupi apewe chakula na yupi akose- WFP

Siku ya wakimbizi duniani ikiwa inaadhimishwa hii leo, shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani, WFP linaonya ni dhahiri shairi kuwa mgao wa chakula kwa wakimbizi utaendelea kupunguzwa kutokana na ongezeko la mahitaji ya kibinadamu sambamba na ukata unaozidi kunyemelea shirika hilo.

Mataifa yaliyoendelea toeni fursa zaidi kwa wakimbizi.

Kuelekea siku ya wakimbizi duniani tarehe 20 juni, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameyahimiza mataifa yaliyoendelea duniani kutoa fursa zaidi kwa wakimbizi wanaosaka makazi mapya.

Chonde chonde ongezeni fedha tunusuru wakimbizi Burkina Faso- UNHCR

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR lina hofu kubwa juu ya ongezeko la mashambulizi na ghasia vinavyofanywa na makundi yalioyjihami dhidi ya raia nchini Burkina Faso.

Zaidi ya watu milioni 100 kote duniani wamelazimika kufungasha virago na kukimbia makazi yao:UNHCR ripoti 

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, lilisema kutokuwa na uhakika wa chakula duniani kote, janga la mabadiliko ya tabianchi, vita nchini Ukraine na dharura nyinginezo kuanzia Afrika hadi Afghanistan ndio sababu kubwa zilizowafanya watu milioni 100 kufungasha virago na kukimbia makwao.