Wahamiaji na Wakimbizi

Naamka kila siku kwa matumaini ya kuleta mabadiliko japo kwa mtu mmoja:Mkimbizi Mahasin Khattab 

 Kutana na mkimbizi kutoka Syria ambaye sasa anaishi kwenye kambi ya wakimbizi wa ndani ya Atma iliyoko karibu na mpaka wa Uturuki. Pamoja na madhila yote aliyopitia anapata faraja anapoweza kubadili maisha japo ya mkimbizi mmoja kwa ushauri nasaha anaotoa kwa maelfu ya wakimbizi kambini hapo

UNHCR iko tayari kuanza tena utoaji wa misaada kwa waliofurushwa Tigray 

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, liko tayari kuanza tena shughuli zake kamili za kibinadamu katika mkoa wa Tigray, Ethiopia mara tu hali itakaporuhusu, kufuatia makubaliano ya kurejesha upatikanaji, ameeleza hii leo msemaji wa shirika hilo Babar Baloch katika mkutano wake na vyombo vya habari mjini Geneva Uswisi.  

UNHCR yaitaka Ethiopia kuruhusu kufikiwa wakimbizi 96,000 wasio na chakula Tigray

Shirika la Umoja wa Mastaifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR leo limeiomba serikali ya Ethiopia kulipa ruhusa ya dharura ili kuweza kuwafikia wakimbizi 96,000 kutoka Eritrea waliokwama kwenye jimbo la Tigray ambao sasa hawana huduma muhimu ikiwemo chakula kutokana na machafuko yanayoendelea kwa mwezi mmoja sasa. 

Wakimbizi wa Ethiopia sasa ni zaidi ya 43,000, Mkuu wa UNHCR atembelea Kartoum Sudan kutathimini hali.

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, Filippo Grandi yuko ziarani nchini Khartoum, Sudan kuangazia hali ya wakimbizi wa Ethiopia ambao hadi sasa zaidi ya 43,000 wameingia mashariki mwa Sudan wakitokea jimbo la Tigray.  

Kwa waliopitia GBV msaada wa kibinadamu pekee hautoshi wanahitaji pia wa kisaikolojia:Razia

Kutana na mwanamke mwanasheria na mwanaharakati wa haki za wanawake Razia Sultana ambaye ameanzisha mahala salama kwenye kambi ya Cox’s Bazaar nchini Bangladesh kwa ajili ya kuwapa msaada wa kisaikolojia wanawake wakimbizi wa Rohingya kutoka Myanmar waliopitia ukatilia wa kijinsia au GBV.

Idadi ya wanaokimbia Tigray Ethiopia kuingia Sudan sasa imezidi 40,000: UNHCR 

Wakati idadi ya watu wanaokimbia jimbo la Tigray nchini Ethiopia kuingia mashariki mwa Sudan sasa imezidi 40,000, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR linafanya jitihada kupata msaada wa kutosha unaohitajika kwa watu hao walio katika uhitaji mkubwa. 

COVID-19 yawa mzigo mkubwa kwa wakimbizi Misri 

Kabla ya janga la ugonjwa wa Corona au COVID-19, idadi kubwa ya wakimbizi nchini Misri walikuwa tayari katika hali ya hatari katika kujikwamua maisha yao. Sasa na janga la Corona, wengi wao wamepoteza vyanzo vyao vya kipato na wanahaha kukimu mahitaji yao ya msingi. 

Kutoka Libya hadi Rwanda, wahamiaji waeleza matumaini mapya 

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limesafirisha kundi la wahamiaji 79 kutoka Libya kwenda Rwanda, ikiwa ni sehemu ya kuhamisha wahamiaji walio hatarini zaidi kwenda maeneo salama. 

Wahamiaji wengi wazidi kupoteza maisha wakikimbilia Ulaya kupitia visiwa vya Canary- IOM 

Shirika la uhamiaji la Umoja wa Mataifa, IOM limeeleza wasiwasi mkubwa juu ya ongezeko la vifo vya wahamiaji vinavyotokea wakati wakisafiri kutoka pwani za Afrika kueleka visiwa vya Canary barani Ulaya. 

Makazi ya ulinzi wa raia yameanza kuwa makazi ya wakimbizi wa ndani Sudan Kusini:UNMISS 

Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS umeshaanza rasmi kuyageuza makazi ya ulinzi wa raia (POCs) na kuwa makambi ya kawaida ya wakimbizi wa ndani kama ulivyoahidi.