Wahamiaji na Wakimbizi

Kimsingi UNHCR haitakiwi iwepo iwapo tutatimiza wajibu wetu- Grandi

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) limetimiza miaka 70 tangu kuanzishwa kwake ambapo Kamishna Mkuu wa shirika hilo Filippo Grandi amesema “niondoeni kwenye jukumu hili”  kwa kushughulikia visababishi vya mamilioni ya watu kukimbia makwao kutokanana vita na ukosefu wa usalama.

Watoto zaidi ya milioni 2 hawajafikiwa na msaada Tigray machafuko yakiendelea:UNICEF 

Watoto wapatao milioni 2.3 kwenye jimbo la Tigay nchini Ethiopia bado hawajafikiwa na msaada wa kibinadamu huku machafuko yaliyoanza mwezi Novemba mwaka huu yakiendelea limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF. 

UNHCR yalaani shambulio nchini Niger katika mji unaohifadhi wakimbizi. 

Shirika la Umoja wa Maraifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, linalaani shambulio llilotekelezwa na washambuliaji wenye silaha huko Toumour, mji ulioko kusini-mashariki mwa Niger, shambulio ambalo limeua watu 28 na kujeruhi mamia wengine. 

WFP imelifungua tena soko la wakulima Cox's Bazar baada ya kulifunga sababu ya COVID-19 

Shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa WFP wiki hii limelifungua  tena soko kubwa la wakulima kwenye kambi ya wakimbizi wa Rohingya ya Cox’s Bazar nchini Bangladesh baada ya kulifunga kwa miezi kadhaa kufuatia mlipuko wa janga la corona au COVID-19. Soko hilo ambalo ni sehemu ya mradi wa WFP ni neema sio tu kwa wakimbizi bali pia jamii inayowahifadhi.

Heko Kenya kwa kuamua kuwapatia uraia wenye asili ya Rwanda na Zimbabwe- UNHCR 

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) limekaribisha uamuzi wa serikali ya Kenya wa kuwapatia utaifa  jumla ya watu 2,970 ambao awali hawakuwa na utaifa wowote na hivyo kushindwa kupata huduma za msingi ikiwemo elimu, afya na ajira. 

Pengo la ujira kwa wahamiaji, linaongezeka katika nchi nyingi za kipato cha juu 

Ujira wa wahamiaji ugenini kwa wastani ni chini ya asilimia 13 kulinganisha na wafanyakazi wenyeji katika nchi za kipato cha juu, imesema ripoti mpya ya shirika la kazi la Umoja wa Mataifa, ILO, iliyotolewa leo mjini Geneva, Uswisi. 

WFP yaendelea kutoa chakula kwa wakimbizi wanaovuka kuingia Sudan wakitokea Tigray  

Shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa, WFP, hii leo mjini Geneva Uswisi limeeleza kuwa  hadi kufikia sasa limeweka vituo sita vya usambazaji wa uhifadhi wa chakula na misaada mingine muhimu ya kibinadamu kwa wakimbizi wanapohamia katika kambi mbalimbali nchini Sudan.  

Wakimbizi wa Ethiopia wanaripoti vizuizi vya kufikia usalama nchini Sudan wakati idadi inakaribia 50,000 

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia wakimbizi, UNHCR, kwa kushirikiana na serikali ya Sudan, linasema sasa limesajili wakimbizi takribani 10,000 wa Ethiopia ambao wamevuka mpaka mashariki mwa Sudan, na wengine wakiripoti kulazimika kukwepa vikundi vyenye silaha ili kuufikia usalama. 

Idadi ya watu wanaohama kwa kulazimishwa yavuka milioni 80, COVID-19 nayo ikizidisha machungu

Wakati picha kamili ya mwaka 2020 bado haijafahamika, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, linakadiria kuwa uhamishaji wa kulazimishwa ulimwenguni au ufurushwaji ulizidi milioni 80 katikati ya mwaka, kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa hii leo mjini Geneva Uswisi kuhusu mwenendo wa uhamishaji wa kulazimishwa ulimwenguni.  

Hali ya kibinadamu Tigray bado ni tata mno, wasiwasi ni mkubwa-UN 

Mkurugenzi wa Huduma ya Habari ya Umoja wa Mataifa Alessandra Vellucci, akijibu maswali ya wanahabari hii leo mjini Geneva Uswisi, amesema kwamba Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ana wasiwasi kuhusu hali ya sasa katika mkoa wa Tigray nchini Ethiopia.