Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR leo limefanikiwa kulihamisha kundi la waomba hifadhi 130 waliokuwa hatarini nchini Libya na kuwapeleka kwenye usalama nchini Rwanda, katika awamu ya nne na ya mwisho ya mwisho kwa mwaka huu wa 2020.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limeipongeza serikali ya Chad kwa kupitisha kwa mara ya kwanza sheria ya kuomba hifadhi ambayo itaimarisha ulinzi kwa karibu wakimbizi 480,000 wanaohifadhiwa nchini humo hivi sasa.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR pamoja na wadau 30 wa kibinadamu hii leo wanatoa wito wa dharura kupatiwa wa dola milioni 156.
Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limewasaidia wakimbizi 3,000 kutoka Mali kurejea kambi ya Goudoubo nchini Burkina Faso miezi tisa baada ya ukosefu wa usalama kuwalazimisha kuhama.
Takwimu za utafiti mpya uliochapishwa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF zinaonyesha kwamba katika nchi zote duniani wahamiaji na watoto waliotawanywa hawahusishwi katika hatua za kitaifa za kupambana na kujikwamua na janga la corona au COVID-19 na wanakabiliwa na upungufu mkubwa wa fursa za huduma muhimu.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) limetimiza miaka 70 tangu kuanzishwa kwake ambapo Kamishna Mkuu wa shirika hilo Filippo Grandi amesema “niondoeni kwenye jukumu hili” kwa kushughulikia visababishi vya mamilioni ya watu kukimbia makwao kutokanana vita na ukosefu wa usalama.
Watoto wapatao milioni 2.3 kwenye jimbo la Tigay nchini Ethiopia bado hawajafikiwa na msaada wa kibinadamu huku machafuko yaliyoanza mwezi Novemba mwaka huu yakiendelea limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF.
Shirika la Umoja wa Maraifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, linalaani shambulio llilotekelezwa na washambuliaji wenye silaha huko Toumour, mji ulioko kusini-mashariki mwa Niger, shambulio ambalo limeua watu 28 na kujeruhi mamia wengine.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) limekaribisha uamuzi wa serikali ya Kenya wa kuwapatia utaifa jumla ya watu 2,970 ambao awali hawakuwa na utaifa wowote na hivyo kushindwa kupata huduma za msingi ikiwemo elimu, afya na ajira.
Ujira wa wahamiaji ugenini kwa wastani ni chini ya asilimia 13 kulinganisha na wafanyakazi wenyeji katika nchi za kipato cha juu, imesema ripoti mpya ya shirika la kazi la Umoja wa Mataifa, ILO, iliyotolewa leo mjini Geneva, Uswisi.