Wahamiaji na Wakimbizi

Udaktari ni wito na ukiwa wako huchoki:Dkt. Wambugu

Kazi ya udaktari kama ilivyo ya ukunga au uuguzi ni wito na wakati majanga kama hivi sasa la virusi vya corona au COVID-19 umuhimu wake unakuwa hauna kifani. Kutana na daktari ambaye pampja na wenzae wanafanya kila wawezalo kuwakinda wakimbizi kambini Kakuma Kenya dhidi ya janga hilo.

COVID-19 si ukomo wa masomo kwa wakimbizi

Nchini Kenya matangazo ya shule kwa njia ya redio sasa yameanza katika kambi za wakimbizi ambapo walimu wanafundisha masomo kupitia redio za jamii ili wanafunzi waendelee na masomo hata wakati huu wa kusalia nyumbani kutokana na janga la ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19.

Asante UNHCR huduma ya kangaroo imeokoa watoto wetu:Wakimbizi

 Huduma ya rahisi lakini muhimu ya kangaroo ambayo inatolewa kwenye kambi ya wakimbizi ya Gado nchini Cameroon imekuwa mkombozi wa wa Maisha ya watoto wanaozaliwa njiti kambini hapo. 

 

 

IFAD na wadau waepusha mizozano kati ya wakimbizi na wafugaji Niger

Nchini Niger, mfuko wa maendeleo ya kilimo, IFAD na wadau wake wamesaidia ujenzi wa mradi wa maji uliosaidia kupunguza mzozano kati ya wakimbizi wa ndani, wafugaji na familia zinazohamahama.

Kila mwanasesere nitengenezaye ni uponyaji dhidi ya machungu niliyopitia- Mkimbizi

Baada ya kubakwa na waasi huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na wazazi wake kuuawa kisha kupata hifadhi nchini Msumbiji, mkimbizi Kituza sasa anatumia wanasesere anaotengeneza si tu kwa kujipatia kipato bali pia kupata uponyaji na kusahau machungu aliyopitia.

Linapokuja suala la wakimbizi na COVID-19 ni bora kukinga kuliko kuponya:UNHCR

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na wadau wake nchini Bangadesh wanachukua kila tahadhari ili kuhakikisha maelfu ya wakimbizi wa Rohingya kwenye moja ya makazi makubwa kabisa ya wakimbizi duniani  ya Cox's Bazaar wanalindwa dhidi ya mlipuko wa Corona au COVID-19.

UNHCR yaongeza juhudu kunusuru maisha ya mamilioni Afrika dhidi ya COVID-19

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema linafanya kila juhudi kuhakikisha linanusuru maisha ya mamilioni ya watu ukanda wa Afrika Magharibi na Kati yaliyo hatarini kutokana na changamoto mpya iliyozuka ya virusi vya Corona au COVID-19.

Tuko watu tisa katika chumba kimoja, tunaihofia COVID-19- Qusai Al-Khatib

Wakati janga la COVID-19 likiendelea kuuzingira  ulimwengu, familia za raia wa Syria zilizoko hatarini zina hofu zaidi kwa sababu zinaendelea kuishi katika mazingira yenye msongamano mkubwa na kukiwa na nafasi finyu ya kupata huduma za afya.

Ni wajibu wetu kuwalinda wakimbizi dhidi ya COVID-19-UNHCR

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema linachukua tahadhari zote na kufanya kila liwezalo ili kuwalinda wakimbizi walio katika makambi mbalimbali ya wakimbizi barani Afrika dhidi ya janga la virusi vya Corona, COVID-19.

UNHCR yajipanga mapema kudhibiti COVID-19 katika kambi za wakimbizi wa Rohingya

Pamoja na kuwa hakuna mgonjwa yeyote wa virusi vya corona, COVID-19 ambaye ameripotiwa miongoni mwa wakimbizi nchini Bangladesh, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linachukua hatua za kujiandaa kukabiliana na mlipuko ikiwemo kujenga wodi za kuwatibu wagonjwa katika maeneo hayo.