Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na wahamiaji, IOM, hii leo mjini Abyei Sudan Kusini, wametoa taarifa ya kufikisha misaada kwa manusura wa mashambulizi yaliyofanyika jumatano iliyopita katika mji wa Kolom, kilomita tisa kutoka mji wa Abyei.