Wahamiaji na Wakimbizi

Hali ndani ya kambi ni mbaya sembuse Rakhine? Wahoji warohingya

Baada ya ziara ya siku sita nchini Myanmar, Afisa mwandamizi wa Umoja wa Mataifa anaona kabisa ya kwamba wakimbizi wa Rohingya walioko Bangladesh bado wana hofu kubwa ya kurejea nyumbani ingawa jitihada za mazungumzo zinaendelea ili warejee Myanmar.

Watendeeni wema wahamiaji Yemen- UNHCR

Umoja wa Mataifa una wasiwasi mkubwa juu ya madhila yanayokumba wahamiaji, wasaka hifadhi na wakimbizi wapya nchini Yemen. Yaelezwa manusura  hufyatuliwa risasi, hupigwa kila mara, hubakwa na hata huvuliwa nguo na kusalia uchi.

 

Ulemavu hautuzuii kubadili maisha yetu

Dhana potofu kuwa ulemavu ndio ukomo wa maisha imetupiliwa mbali huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Wakimbizi wa kike na wa kiume kutoka Burundi wamechukua hatua.

Baada ya miaka 38 ya ndoa si kifo bali vita vyawatenganisha wanandoa

Pater Juma Maru na Cecilia Ofowa ni wanandoa kwa miaka 38, raia hawa wa Sudan Kusini hivi sasa ni wakimbizi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, ingawa wanaonana , lakini hawawezi kuishi pamoja kama mke na mume kulikoni?

Licha ya safari za kukata tamaa kupungua, hatari ipo palepale :UNHCR

Licha ya kupungua kwa idadi ya wakimbizi na wahamiaji wanaokwenda kusaka hifadhi Ulaya , hatari zinazowakabili njiani watu hao kwa kiasi fulani zimeongezeka, kwa mujibu wa ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR. 

Tujitathmini kabla ya kunyooshea vidole wahamiaji

Je wangapi kati yetu ndani ya familia zetu tuna historia ya uhamiaji zinazoimarisha urithi wa tamaduni zetu?

Kampeni ya mshikamano na wakimbizi yang’oa nanga

Siku ya kimataifa ya michezo kwa maendeleo na amani yaangaziwa huku kampeni maalum ikizinduliwa.

Licha ya mzozo, DRC yakirimu wakimbizi- UNHCR

Umoja wa Mataifa umejionea miradi dhahiri ya kilimo, ufugaji na biashara inayotekelezwa huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kwa ajili ya kuwajengea uwezo wakimbizi wanaotoka nchi jirani.

Wahamiaji watarajie nini kutoka Brussels?

Kila uchao manyanyaso wapatayo wahamiaji  yanaripotiwa kila kona ya dunia, na sasa Umoja wa Mataifa pamoja na Muungano wa Ulaya wameamua kuchukua hatua.

Sola yawaangazia nuru wakimbizi wa ndani Ethiopia: IOM

Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM kwa ushirikiano na kampuni ya Panasonic Solar Lanterns, wametoa msaada wa umeme unaotumia nishati ya jua au wa sola kwa zaidi ya  wakimbizi wa ndani 2400 nchini Ehtiopia.