Nchini Bangladesh shirika la mpango wa chakula duniani, WFP linashirikiana na warohingya waliosaka hifadhi humo katika kuandaa vema makazi na uhifadhi wa chakula wakati huu ambapo msimu wa pepo za monsuni unabisha hodi.
Watoto 55,000 wanakadiriwa kuwa katika hatari kubwa ya mafuriko na maporomoko ya udongo kwenye makazi ya wakimbizi wa Rohingya nchini Bangladesh limeonya leo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF.
Baada ya kupitia machungu na mateso makali korokoroni nchini Libya hatimaye wakimbizi 56 kutoka mataifa mbalimbali wamepewa hifadhi ya kudumu kwenye makazi ya watawa wa kikatoliki wa shirika la wafransisca kaskazini mashariki mwa Ufaransa.
Umoja wa Mataifa umeisihi Ugiriki iboreshe mazingira na kasi ya mapokezi ya wasaka hifadhi kwenye mkoa wa Evros ambako wakimbizi wanazidi kumiminika wakipitia mpaka wa nchi hiyo na Uturuki.
Hatua ya kutoa mafunzo ya teknolojia ya habari na mawasiliano au TEKNOHAMA kwa wakimbizi kupitia shule ya ReDi nchini Ujerumani, imefufua matumaini ya mustakhbali wao waliokuwa wameukatia tamaa.
Baada ya mashauriano na mazungumzo na pia kusikia kauli kutoka kwa wawakilishi wa wananchi wa Syria, wahisani wamefungua pochi zao na kuchangisha fedha kukuwamua wananchi hao ambao mustakhabali wao uko mashakani.
Kuimarika kwa hali ya usalama jimboni Darfur nchini Sudan kumesababisha awamu ya kwanza ya wakimbizi waliosaka hifadhi nchini Chad kurejea jimboni humo wiki hii.
Awali wananchi walipata shida kufika polisi ili kueleza madhila yao, lakini hivi sasa Umoja wa Mataifa umeweka mazingira ambamo kwayo wananchi wanaripoti polisi madhila yanayowakumba kwa urahisi na pia bila gharama yoyote.