Licha ya vita vinavyoendelea na changamoto nyingine lukuki nchini Sudan Kusini, Daktari mmoja bingwa wa upasuaji nchini humo amedhamiria kufanya kila awezalo kuokoa maisha ya maelfu ya wakimbizi wa ndani nchini humo, huku akifanya kazi katika mazingira magumu yaliyomfanya kutunukiwa tuzo ya wakimbizi mwaka huu.