Wahamiaji na Wakimbizi

Warohingya wahamishiwa makazi salama zaidi

Baada  ya miezi kadhaa ya kujaza udongo na kunyanyua maeneo ya ardhi ili kuwa na eneo tambarare, hatimaye baadhi ya wakimbizi warohingya huko Bangladesh sasa wana amani kwani ujio wa mvua za pepo za monsuni sasa si tishio tena kwa uhai wao.

Miaka 20 ya kuchunguza maiti ili kuleta nuru kwa familia

Profesa mmoja nchini Ugiriki ameamua kutumia ubobezi wake wa utambuzi wa maiti ili kuweza kuwaunganisha na ndugu zao baada ya ndoto zao za kusaka maisha bora Ulaya kuishia kwenye mto mmoja unaotenganisha Ugiriki na Uturuki.

Fedha za wahamiaji hukwamua nchi zao za asili- UNCTAD

Ingawa wanaishi ughaibuni, wahamiaji bado wanachangia kiuchumi kwenye nchi walizotoka. Nchi hunufaika, halikadhalika familia zao.

Hadithi za wakimbizi wanaorejea kutoka Libya zitatia uchungu: Grandi 

Kamishina mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya wakimbizi Filippo Grandi, amesafiri usiku kucha hadi nchini Niger akiambatana na wakimbizi zaidi ya 100 wengi wakiwa wanawake na watoto, waliosafirishwa kutoka kwenye kituo walichokuwa wanashikiliwa nchini Libya. 

Siku ya wakimbizi ni siku ya kutambua utu kwa vitendo: Grandi

Siku ya wakimbizi duniani ni siku ya kutambua utu kwa vitendo na pia kushikamana na wakimbizi na jamii zinazowahifadhi, amesema Kamishina mkuu wa wakimbizi wa Umoja wa Mataifa Filippo Grandi. 

Bado ukata waathiri wakimbizi na wenyeji Uganda- UNHCR

Uganda yafungua milango kwa wakimbizi, wahisani nao wasuasua kufungua pochi zao ili kusaidia operesheni za usaidizi.

Je wafanya nini kukabili janga la wakimbizi?

Ungalifanya nini iwapo ungelazimishwa kuondoka nyumbani kwako?

Hifadhi ya ukimbizi wangu iko katika soka:Abdi

Wakati michuano ya kombe la dunia iking’oa nanga hii leo nchini Urusi na kukutanisha mamilioni ya watu, vijana barubaru wakimbizi kutoka Afrika mashariki waishio hapa Marekani wamesema kabumbu imewasahaulisha ukimbizi .

Zaidi ya wahamiaji milioni 2.5 walisafirishwa kimagendo 2016- UNODC

Utafiti kutoka ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kudhibiti madawa ya kulevya na uhalifu, UNODC, umebaini kuwa zaidi ya wahamiaji milioni 2.5 walisafirishwa kimagendo mwaka 2016.

Chondechonde wapokeeni wahamiaji waliokwama melini Mediterranea UNHCR

Shirika la kuwahudumia wakimbizi duniani UNHCR limeziomba serikali husika  kuwakubalia mamia ya watu ambao wamekwama katika bahari ya Mediterani wakiwa ndani ya meli ya  the Aquarius kuingia nchini mwao.