Masuala ya hofu kuwa mtaji wa kisiasa, kauli za chuki, ukosefu wa usawa, ushirikiano wa kimataifa, mabadiliko ya tabianchi, maandamano huko Sudan na kwingineko duniani ni miongoni mwa mambo ambayo yamebeba mkutano kati ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres na waandishi wa habari hii leo mjini New York, Marekani.