Sheria na Kuzuia Uhalifu

Kesi ya waziri aliyetuhumiwa makosa ya jinai ya halaiki Rwanda yaanza kusikilizwa na ICTR

Kesi ya aliyekuwa Waziri wa Mipango ya Maendeleo katika Rwanda, yaani Augustin Ngirabatware, imeanza kusikilizwa rasmi leo Ijumatano kwenye Mahakama ya Kimataifa juu ya Rwanda (ICTR).

Aliyekuwa ofisa wa serikali Rwanda akiri shtaka la makosa ya vita

Michael Bagaragaza, aliyekuwa mkuu wa ofisi ya viwanda vya chai katika Rwanda leo amekiri shtaka la makosa ya jinai ya vita baada ya kutuhumiwa kushiriki kwenye mauaji ya halaiki nchini mwao katika 1994.

Baraza la Haki za Binadamu linazingatia athari za taka za sumu kwa raia Cote d'Ivoire

Mkariri Maalumu mwenye kutetea haki za binadamu, Olechukwu Ibeanu, amewasilisha ripoti mbele ya Baraza la Haki za Binadamu linalokutana Geneva, iliozingatia athari za taka za sumu zilizotupwa na makampuni ya kigeni katika Cote d\'Ivoire mnamo mwezi Agosti 2006.

Idadi ya vifo kupanda kwa wahamiaji Waafrika waliojaribu kuvuka Ghuba ya Aden

Mnamo saa 48 zilizopita imeripotiwa na Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) kwamba watu 16 walifariki na 49 wengine wamepotea, na kudhaniwa ni maututi kwa sababu ya matukio matatu tofauti yanayoambatana na mashua zilizokuwa zikivusha watu kimagendo kwenye Ghuba ya Aden wahamiaji waliojumlisha wale waliotoka Usomali na raia wengine wa kutoka Afrika.

Utaratibu uliofungamana kimataifa wapendekezwa na UM kukabili uharamia katika mwambao wa Usomali

Imehadharishwa na mtaalamu wa UM kwamba mafanikio haba yaliopatikana katika udhibiti wa vitendo vya uharamia nje ya mwambao wa Usomali humaanisha kunahitajika mwelekeo mpya kukabiliana na tatizo hili badala ya kulenga kadhia hizi baharini pekee.

Jaji mpya kutoka Urusi kuapishwa na ICTR

Mnamo siku ya leo, kwenye Mahakama ya Kimataifa juu ya Rwanda (ICTR) iliopo Arusha, Tanzania aliapishwa Jaji mpya wa kutoka Shirikisho la Urusi, Bakhtiyar Tuzmukhamedov.

ICBL yawahimiza wanachama wa UA kusafisha mabomu yaliotegwa Afrika

Taasisi ya Kampeni ya Kimataifa Kupiga Marufuku Mabomu Yaliotegwa Ardhini (ICBL) imetoa taarifa maalumu kwenye mkutano wa kikanda, iliokuwa na makusudio ya kuwahamasisha wanachama wa Umoja wa Afrika (UA) kuongeza jitihadi zao kwenye huduma za kukomesha na kufyeka milele kutoka bara la Afrika, zile silaha za miripuko zilizotegwa ardhini, na pia kuhakikisha haki za wanusurika wa silaha hizo zinahishimiwa kikamilifu.

Mahakama ya Rufaa ya ICC imeamua aliyekuwa kiongozi wa JKK asalie kizuizini wakati akisubiri kesi

Mahakama Ndogo ya Rufaa ya Mahakama ya Kimataifa Juu ya Jinai ya Halaiki (ICC) imeamua Jean-Pierre Bemba Gombo, aliyekuwa Naibu Raisi wa JKK, aendelee kuwekwa kifungoni kabla ya kesi yake kusikilizwa na Mahakama Kuu.

Maharamia wa uvuvi watanyimwa makimbilio salama baada ya kufikiwa maafikiano mapya ya kimataifa

Mataifa Wanachama 91 wa Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) yameafikiana kuukubali waraka wa mwisho wa mkataba wa kimataifa uliokusudiwa kupiga vita uvuvi haramu kwenye maeneo yao.

Mapigano makali Mogadishu yanaathiri zaidi raia, inasema OCHA

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imeripoti kutoka Geneva kwamba mapigano makali yaliopamba kwenye mji wa Mogadishu, Usomali yanaendelea kuathiri kwa wingi raia.