Sheria na Kuzuia Uhalifu

Utekaji nyara wa misaada ya kihali Usomali umelaumiwa vikali na UNICEF

Imetangazwa na Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) kuwa inalaani, kwa kauli kali, utekaji nyara pamoja na uharibifu wa misaada ya kiutu na majengo yake, ulioripotiwa kuendelezwa na majeshi ya mgambo kwenye mji wa Jowhar katika Usomali.

Mashitaka mapya dhidi ya Aung San Suu Kyi yalaumiwa na Navi Pillay

Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu, Navi Pillay, Ijumaa alishtumu taarifa zilizoonyesha kwamba wenye mamlaka Myanmar walimfungulia mashitaka mapya mpinzani, Aung San Suu Kyi. Aliwasihi kufuta msururu wa mashitaka ambayo yanafungamana na tukio nje ya uwezo wa Aung San Suu Kyi.

UNHCR na Wakf wa Mandela waazimu kupiga vita bia chuki za wageni Afrika Kusini

Shirika la UM Linalohudumia Wahamiaji (UNHCR) pamoja na Taasisi ya Wakf wa Nelson Mandela (NMF) wamejumuika kwenye kadhia muhimu ya kupiga vita lile janga la hatari kuu inayochochea chuki za wazalendo dhidi ya wageni katika Afrika Kusini, tatizo ambalo mwaka jana lilisababisha mauaji ya wageni 62, wingi wao wakiwa wahamiaji kutoka nchi za Afrika pamoja na watu wenye kuomba hifadhi ya kisiasa.