Sheria na Kuzuia Uhalifu

Mkutano wa Brussels juu ya Usomali waahidi mamilioni kufufua amani

Kwenye Mkutano wa Kimataifa juu ya Usomali, uliofanyika kwenye mji wa Brussels, Ubelgiji Alkhamisi ya leo, wenye kuongozwa bia na Mwenyekiti wa UA, Jean Ping na KM wa UM Ban Ki-moon, uliwahamasisha wafadhili wa kimataifa kuahidi kuchangisha karibu dola milioni 250 kulisaidia taifa husika la Pembe ya Afrika kurudisha utulivu na amani ya eneo.

Abiria 35 wa mashua za magendo wameripotiwa na UNHCR kuzama Yemen

Taarifa ya Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) imeeleza kwamba watu 35 waliripotiwa kuzama Ijumatano kwenye mwambao wa jimbo la Abyan, Yemen, liliopo kilomita 250 mashariki ya Aden, baada ya moja ya mashua mbili za wafanya magendo kupinduka.

Mjumbe wa KM anabashiria askari watoto wataachiwa na waasi katika JKK

Radhika Coomaraswamy, Mjumbe Maalumu wa KM Anayehusika na Hifadhi ya Watoto kwenye Mazingira ya Mapigano ameripoti kuwepo maendeleo ya kisiasa ya kutia moyo hivi karibuni, katika JKK, ambayo alisema yamewakilisha fursa mpya itakayosaidia kuharakisha kuachiwa huru wale askari watoto waliokuwa wakidhibitiwa na makundi ya waasi wanaochukua silaha.

Mauaji ya mtetezi wa Haki za Binadamu Burundi yalaaniwa na UM

Akich Okola, Mtaalamu Maalumu aliyeteuliwa na Baraza la UM juu ya Haki za Binadamu kuchunguza utekelezaji wa haki za kiutu katika Burundi, ameripoti kuchukizwa sana na taarifa za mauaji ya Ernest Manirumva, Naibu-Raisi mzalendo wa shirika lisio la kiserikali linaloitwa OLUCOME, mauaji yaliotukia mjini Bujumbura, nyumbani mwa Manirumva, mnamo usiku wa tarehe 08 Aprili.

Matishio yanayokithiri ya uhalifu wa mipangilio yanazingatiwa na Kamisheni ya UM

Kamisheni ya UM Inayohusika na Mahakama za Kesi za Jinai na Udhibiti wa Uhalifu Alkhamisi imefungua rasmi mjini Vienna, kikao cha 18 cha wawakilishi wa kimataifa kujadilia taratibu za pamoja, kukabiliana na tishio la uhalifu wa mipangilio dhidi ya utulivu na amani duniani.

Mchango ziada wa kimataifa unahitajika dhidi ya maharamia, asema Mjumbe wa KM kwa Usomali

Mjumbe Maalumu wa KM kwa Usomali, Ahmedou Ould-Abdalla aliwasilisha taarifa maalumu kwa waandishi habari, kufuatia tukio la majuzi kuhusu mapambano na maharamia, nje ya mwambao wa Usomali. Alisema kwenye taarifa kwamba Mataifa Wanachama katika UM yanawajibika kukuza mchango wao katika kukabiliana na kile alichokiita "msiba mkuu wa kimataifa", msiba ambao alidai "husababisha uharibifu mkubwa wa amani ulimwenguni."

Mjumbe wa KM ataka kuchukuliwe hatua kali kimataifa dhidi ya uharamia Usomali

Wapatanishi wa Kimarekani wameripotiwa kujihusisha kwenye mazungumzo na maharamia wa Kisomali, ili kumwachia kapteni wa meli ya Marekani aliyeshikwa sasa hivi kwenye mashua ya kuokolea iliopo katika Bahari ya Hindi.

Mkariri wa UM kuhusu mauaji nje ya mahakama ashtumu vyombo vya sheria Kenya

Profesa Philip Alston, aliye Mkariri Maalumu wa UM dhidi ya Mauaji Nje ya Taratibu za Mahakama amewasilisha ripoti ilioshtumu vikali vyombo vya sheria Kenya, ambavyo alidai hushiriki kwenye vitisho vya mpangilio na mabavu dhidi ya watetezi wazalendo wa haki za binadamu, hasa wale watetezi waliotoa ushahidi kwa tume ya uchunguzi ya UM juu ya ukiukaji wa haki hizo.

Kumbukumbu ya miaka 15 ya mauaji ya Rwanda kuadhimishwa na UM

Kadhalika, tarehe 07 Aprili 2009 inaadhimisha miaka 15 ya mauaji ya halaiki yaliotukia Rwanda katika 1994.