Sheria na Kuzuia Uhalifu

Pombe inaua mtu mmoja kila baada ya sekunde 10 : WHO

•    Ripoti ya WHO yafichua mbinu za ushawishi zinazotumiwa na kampuni za pombe
•    Mbinu hizo zinazidi udhibiti wa matangazo.
•    Watu mashuhuri mitandaoni watumika
•    Mbinu mpya zabuniwa kuwalenga wanawake

Ziara ya Katibu Mkuu wa UN kuhusu Ukraine: “Nafurahia kuripoti mafanikio fulani“

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonip Guterres amelihutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo jioni (05-05-2022) na kueleza kuwa wakati wa ziara yake maalum nchini Urusi na Ukriane hakusita kuwaeleza kinaga ubaga bila kupepesa maneno kwa nyakati tofauti na marais wa nchi hizo kwakuwa anataka kuona mzozo na ukatili unaoendelea sasa unamalizika mara moja. 

Hatari ya kutetea wanawake wanaotuhumiwa kwa uchawi nchini Papua New Guinea

Nchini Papua New Guinea, suala la kuwatetea wanawake wanaotuhumiwa kwa uchawi, imekuwa kazi ya kutishia maisha. 

ICJ yaamua Urusi ikomeshe operesheni zake za kijeshi Ukraine

Urusi isitishe operesheni zake za kijeshi nchini Ukraine, imesema Mahakama ya Umoja wa Mataifa kuhusu haki, ICJ katika uamuzi wake iliyotoa leo huko The Hague, nchini Uholanzi.
 

Kukabili kesi za ukatili wa kingono, tunawafundisha wanawake kutunza Ushahidi- Jaji Okwengu

Dunia ikiwa inaendelea na shamrashamra za mwezi Machi ambao ni mwezi wa wanawake, nchini Kenya, Jaji wa Mahakama ya Rufaa Hannah Okwengu ametaja mafanikio yaliyopatikana tangu kuanza kwa harakati za kuweka jicho la kijinsia katika mahakama.
 

Majaji wanawake huvaa kofia zaidi ya moja ya ujaji- Jaji Okwengu

Mwaka huu wa 2022 kumefanyika maadhimisho ya kwanza ya siku ya majaji wanawake duniani maudhui yakiwa Haki katika mtazamo wa kijinsia, lengo la maudhui hayo likiwa kuchagiza uwepo wa majaji wanawake ili kuhakikisha haki zaidi katika sekta ya mahakama.
 

Uhusiano baina ya mihadarati na mitandao ya kijamii lazima uvunjwe: INCB Ripoti

Bodi ya kimataifa ya kudhibiti madawa ya kulevya (INCB), ambayo ni chombo huru, kinachoungwa mkono na Umoja wa Mataifa, imetoa wito kwa serikali kufanya jitihada zaidi kudhibiti mitandao ya kijamii ambayo inasifu tabia mbaya zinazohusiana na madawa ya kulevya na kuchagiza mauzo ya bidhaa zinazodhibitiwa au kupigwa marufuku.

ICC iko tayari kuanza kuchunguza uhalifu wa kimataifa uliofanywa katika himya ya Ukraine

Mahakama ya Kimataifa ya Makoa ya Jinai (ICC) inaweza kuanza uchunguzi kuhusu vitendo vya mauaji ya halaiki, uhalifu dhidi ya ubinadamu na uhalifu wa kivita uliofanywa katika himaya ya Ukraine.  

UNHCR yashtushwa na ongezeko la mashambulizi dhidi ya wakimbizi DRC

Shirika la Umoja wa Mataifa linalo hudumia wakimbizi UNHCR na washirika wake wameeleza kushtushwa na ripoti za mashambulizi nane makubwa yaliyotokea katika siku 10 za mwanzo wa mwezi Februari mwaka huu 2022 katika jimbo la Ituri nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.

Fahamu ukweli kuhusu ukeketaji(FGM)

Mambo muhimu 
• Ukeketaji unahusisha uondoaji wa sehemu au sehemu yote ya siri ya nje ya mwanamke au kuweka jeraha lingine kwa viungo vya uzazi vya mwanamke kwa sababu zisizo za kimatibabu.