Sheria na Kuzuia Uhalifu

Watu 126 wakhofiwa kufa kwenye Ghuba ya Aden

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR)limeripoti kwamba katika wiki za karibuni watu 126 kutoka Afrika Mashariki walifariki au kupotea walipokuwa wanajaribu kuvuka Ghuba ya Aden baada ya kutupwa majini kutoka meli na mashua za wafanya magendo.

Katibu Mkuu amepeleka ofisa wa hadhi ya juu DRC kuongoza uchaguzi wa uraisi

Naibu KM juu ya Masuala ya Kisiasa, Ibrahim Gambari wiki hii anzuru Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) kwa madhumuni ya kuhakikisha uchaguzi utakaofanyika nchini mwisho wa mwezi kuchagua raisi na pia wawakilishi wa baraza la majimbo utakuwa wa amani.

Mahakama ya ICTR na wanadiplomasiya washauriana na Kenya utaratibu wa kumshika mtuhumiwa wa mauaji ya halaiki

Hassan Bubacar Jallow, Mwendesha Mashitaka wa Mahakama ya UM juu ya Rwanda (ICTR)amefanya mazungumzo mjini Nairobi na wawakilishi wa ofisi za ubalozi 25 pamoja na mawaziri wa Kenya, akiwemo Waziri wa Sheria, Martha Karua kuzingatia juhudi za pamoja za kumshika yule mfanya biashara mtoro wa Rwanda, Felicien Kabuga ambaye alituhumiwa kufadhilia msaada wa kuendeleza mauaji ya halaiki nchini mnamo mwaka 1994.

Serekali ya Uganda kutoa msamaha kwa waasi wa LRA hali ikiruhusu

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Uganda, Sam Kutesa aliwaarifu wajumbe wa kimataifa katika Baraza Kuu kwamba serekali yake, ikilazimika, ipo tayari kutoa msamaha kwa viongozi wa kundi la Lord\'s Resistance Army (LRA), kundi la waasi ambalo linajulikana kwa ukatili wa kuwatumia wanajeshi watoto wanaolazimishwa kuendeleza vitendo vya karaha dhidi ya utu, na pia kuendeleza unyanyasaji wa kijinisia dhidi ya wanawake wanaowateka nyara katika Uganda ya Kaskazini. jafanya askari mtoto ambalo limetuhumiwa, katika siku za nyuma, kuendeleza vitendo vya kikatli vilivyoharamisha haki za kiutu dhidi ya watoto na wanawake.

ICTR imetoa hukumu ya kumwachia huru aliyekuwa Waziri wa Elimu Rwanda

Mahakama ya UM juu ya Rwanda wiki hii iliamua, kwa kauli moja, kumwachia huru Andre Rwamakuba, aliyekuwa Waziri wa Elimu wa Rwanda aliyeshtakiwa kushiriki kwenye mauaji ya halaiki katika 1994. Mahakama iliripoti kuwa ilishindwa kupatiwa ushahidi wa kuridhisha ulioweza kuthibitsha kihakika kwamba Rwamakuba ana hatia.

Liuteni-Kanali Tharcisse Muvunyi wa Rwanda ahukumiwa kifungo cha miaka 25 gerezani

Mahakama ya UM juu ya Rwanda (ICTR) imetoa adhabu ya hukumu ya kifungo cha miaka 25 kwa Liuteni-Kanali Tharcisse Muvunyi, aliyekuwa kamanda wa zamani wa jeshi la Rwanda ambaye alipatikana na hatia ya kushiriki, katika miaka ya 1990s, kwenye mauaji ya halaiki na jinai dhidi ya raia.

Njia za kimagendo katika Ghuba ya Aden

Shirika la UM juu ya Wahamiaji (UNHCR) linabashiria watu wengi watapoteza maisha kutokana na kufumka kwa shughuli hatari za misafara ya magendo ya watu katika Ghuba ya Yemen, umma ambao husafirishwa kutoka Usomali na kupelekwa Yemen.

Maafisa wa usalama Tanzania kumuachilia huru wakili wa utetezi katika ICTR

Maafisa wa usalama katika Tanzania wamemuachia huru yule wakili wa utetezi kwenye mahakama ya kimataifa ya Rwanda, (ICTR) bila ya maelezo juu ya sababu za kukamatwa kwa wakili huyo.

Baraza la Usalama kupeleka jeshi la kulinda amani nchini Sudan

Baraza la Usalama, limekubali kupeleka jeshi la kulinda amani la Umoja wa mataifa la zaidi ya wanajeshi elfu 17 katika jimbo lenye ghasia la Darfur huko Sudan, ifikapo mwisho wa mwaka huu.

Wagombea urais nchini DRC wakubali kuunda tume

Afisi ya Umoja wa mataifa huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, MONUC ilitangaza wiki hii kuwa wagombea wawili walobaki wa kiti cha rais huko kutokana na uchaguzi wa mwezi uliyopita, wamekubaliana kuunda tume ya pamoja kuchunguza ghasia zilizotokea baada ya kutolewa matokeo ya awali,