Sheria na Kuzuia Uhalifu

Mahakama ya ICC yasikiliza kesi yake ya kwanza mjini Hague

Mahakama pekee ya kudumu ya kimataifa juu ya makosa ya jinai ya vita, yaani Mahakama ya ICC ilisikiliza kesi yake ya mwanzo Alkhamisi, Novemba tisa(2006), iliofanyika mjini Hague, Uholanzi inayohusika na Thomas Lubanga Dyilo, aliyekuwa jemadari wa kundi la wanamgambo wa kundi la Forces Patriotiques pour la Liberation du Congo (FPLC) katika wilaya ya Ituri, Mashariki-kaskazini ya JKK katika miaka ya 2002-03.

Shirikisho la Urusi kusaidia Kenya kukabilina na ukame

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limefadhiliwa msaada wa dharura wa dola milioni 2 kutoka Shirikisho la Urusi utakaotumiwa kwenye operesheni za kuwapatia chakula watu milioni 3 nchini Kenya, walioathirika na tatizo la ukame.

KM anaamini Afrika itafaidika kimaendeleo ikijifunza namna ya kupunguza ufukara kutoka kwa Wachina

KM wa UM Kofi Annan ameipongeza Uchina kwa kuahidi kuongeza, kwa mara mbili zaidi, misaada ya maendeleo kwa bara la Afrika itakapotimia 2009. Ahadi hii ilifikiwa na wawakilishi wa Serekali ya Uchina na viongozi wa Afrika waliohudhuria Mkutano Mkuu wa Baraza la Ushirikiano wa Uchina na Afrika uliofanyika majuzi mjini Beijing.

UNICEF yaanzisha mchezo wa kompyuta kusaidia vijana wa Afrika Mashariki kupiga vita UKIMWI.

Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) wiki hii limewakilisha rasmi mchezo mpya wa kompyuta, kwa lugha ya Kiswahili, unaopatikana kwenye mtandao, uliokusudiwa kutumiwa na vijana ili kuwasaidia kwenye zile juhudi za kujifunza mfumo unaoridhisha wa maisha ili, hatimaye, wafanikiwe kujikinga na hatari ya maambukizo ya virusi maututi vya UKIMWI. ~~

Mashambulio na mauaji yaliyofanywa na wanamgambo karibuni katika Darfur yashtumiwa vikali na KM

KM Kofi Annan ametoa taarifa maalumu, kwa kupitia msemaji wake,iliyoshutumu vikali mashambulio ya hivi karibuni ya kundi moja la wanamgambo wa Sudan yaliyofanyika katika makazi ya eneo la Jebel Moon, Darfur ya Magharibi ambapo iliripotiwa makorja ya raia waliuawa, ikijumuisha pia watoto wadogo. Mashambulio haya yaliwalazimisha maelfu ya raia kuhajiri mastakimu kunusurisha maisha.

Jan Pronk ataendelea kuwa Mwakilishi Maalumu wa UM kwa Sudan

Wiki hii KM Kofi Annan alikutana kwa mashauriano na Jan Pronk, Mjumbe wake maalumu anayeongoza lile Shirika la Ulinzi wa Amani la UM nchini Sudan, yaani UNMIS. Hivi majuzi Serekali ya Sudan iliripotiwa kumpiga marufuku Pronk kuwepo nchini.

UM unahimiza hali ya utulivu iendelezwe katika DR Congo wakati wa duru ya pili ya uchaguzi wa uraisi

UM umetoa nasaha kwa wale viongozi wenye kugombea kiti cha uraisi katika Jamhuriya Kidemokrasi ya Kongo (DR Congo), kwenye duru ya pili ya uchaguzi utakaofanyika mwisho wa wiki [Ijumapili], kuendelea kuheshimu muungano wa taifa kabla na baada ya upigaji kura kumalizika, bila ya kuzusha mfarakano kutokana na tofauti za kimawazo.

Baraza la Usalama kuridhia kuanzishwa ofisi ya kuimarisha amani Burundi

Baraza la Usalama limepitisha, kwa kauli moja, azimio la kuanzisha ofisi maalumu mpya nchini Burundi (Bureau Integre des Nations Unies au Burundi, BINUB)itakayopewa dhamana ya kusaidia kujenga utulivu wa kudumu nchini baada ya Shirika la UM juu ya Ulinzi wa Amani (ONUB) kukamilisha operesheni zake mwisho wa mwaka (31 Disemba 2006).

Eritrea yashtumiwa kuharamisha mapatano ya kusitisha mapigano mipakani

KM Kofi Annan akijumuika na Baraza la Usalama wiki hii wametoa taarifa ya pamoja kuishtumu Eritrea kwa kupeleka vifaru 15 na pia wanajeshi karibu 1,500 kwenye lile Eneo la Muda la Usalama (TSZ) liliopo mipakani na Ethiopia.

Watu 126 wakhofiwa kufa kwenye Ghuba ya Aden

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR)limeripoti kwamba katika wiki za karibuni watu 126 kutoka Afrika Mashariki walifariki au kupotea walipokuwa wanajaribu kuvuka Ghuba ya Aden baada ya kutupwa majini kutoka meli na mashua za wafanya magendo.