Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo Jumatano limekutana kujadili kuhusu kufungwa kwa ujumbe wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya usaidizi wa haki nchini Haiti MINUJUSTH, hapo mwezi Oktoba mwaka huu.
Tatizo la mabomu ya kutegwa ardhini ni kubwa nchini Sudan Kusini kutokana na vita vinavyoendelea, na mabomu hayo ni tishio kwa maisha na usalama wa watu, hata hivyo Umoja wa Mataifa nchini humo unasema inawezekana kuchukua hatua na kumaliza mabomu hayo.
Mtaalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa kupitia ripoti iliyochapishwa hii leo na baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa, ameeleza kusikitishwa kwake na hukumu ya miaka mitano zaidi dhidi ya Jaji Maria Lourdes Afiuni wa Venezuela.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limesikitishwa na kughadhibishwa na kitendo cha watoto kuendelea kulipa gharama kubwa ya maisha yao kwenye mgogoro wa Mali.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wake hii leo mjini New York Marekani, amesema amesitushwa na ripoti kuwa takribani watu 134 wakiwemo watoto na wanawake wameuawa na watu wengine takribani 55 kujeruhiwa kufuatia shambulio lililotekelezwa mapema leo jumamosi katika kijiji cha Ogossagou Peulh,Mopti katikati mwa Mali.
Umefika wakati wa kusema sasa imetosha, ubaguzi wa rangi , chuki dhidi ya wageni na mifumo mingine yoyote ya chuki na ubaguzi haina nafasi katika karne hii, amesema Kamishina Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet.
Shirika la Mpango wa chakula duniani (WFP) linashirikiana na serikali ya Uganda kuchunguza kilichosababisha kuugua kwa watu zaidi ya 282 baada ya kupokea msaada wa chakula aina ya nafaka kutoka kwa WFP.
Muungano wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, mashirika ya Umoja wa Mataifa na wataalam wa haki za binadamu wanaokutana kwa ajili ya mkutano wa tume ya masuala ya madawa ya kulevya mjini Vienna Australia, leo umezindua viwango vipya vya kimataifa vya kisheria ili kuandaa na kubadili mtazamo wa vita vya kimataifa dhidi ya tatizo la mihadarati.
Bodi ya kimataifa ya kuzuia madawa ya kulevya INCB imeonya kuwa progamu dhaifu ya matumizi ya bangi kwa ajili ya kupunguza maumivu huenda ikasababisha ongezeko la matumizi zaidi ya bangi kwa uraibu.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani vikali shambulio la kigaidi lililotokea Alhamisi mjini Moghadishu nchini Somalia na kukatili maisha ya watu wengi.