Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu ukatili wa kingono kwenye mizozo, Pramila Patten amekaribisha uamuzi wa Mahakama ya Juu huko Koblenz, Ujerumani, dhidi ya kanali wa zamani wa Syria Anwar R. kuhusu uhalifu dhidi ya kibinadamu ikiwa ni pamoja na vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia.