Mwaka 2020 ulikuwa ni mwaka wa majanga lakini 2021 ni mwaka wa fursa na matumaini! Ni kauli ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres aliyotoa leo kwa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani akielezea vipaumbele vyake 10 kwa mwaka 2021.
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mtaifa la kuhudumia watoto UNICEF, Henrietta Fore amelaani vikali shambulizi ambalo limetekelezwa jana na kuua wananchi wakiwemo watoto katika mji wa Mozogo, kaskazini mwa Cameroon.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema ameshtushwa na hali iliyoendelea leo mjini Washington DC nchini Marekani na kuwataka viongozi wa kisiasa kuwaasa wafuasi wao kujizuia na ghasia.