Sheria na Kuzuia Uhalifu

Matokeo ya uchunguzi kuhusu ndege ya MH17 yanasikitisha-Guterres

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres amesikitishwa na ripoti mpya kuhusu kutunguliwa kwa ndege ya abiria ya Malaysia MH17.

Vita dhidi ya ufisadi ni chachu kwa SDGs

Rushwa ni adui wa haki, ni kauli ambayo hii leo imepatiwa mkazo wakati wa maadhimisho ya miaka 15 ya mkataba wa kimataifa wa kupambana na rushwa duniani.

Ulinzi wa raia vitani- maneno mengi kuliko vitendo

Mizozo kote duniani inaibua vitisho na machungu kwa mamilioni ya raia wakiwemo wanawake, wasichana, wanaume, wavulana na watoto.

Miaka 70 ya Tume ya sheria ya UN yaleta nuru

Tume ya sheria ya Umoja wa Mataifa mwaka huu inatimiza miaka 70 tangu kuanzishwa kwake ambapo imeelezwa kuwa uwepo wake umekuwa na mafanikio makubwa. 

Baraza lataka uchunguzi wa kilichotokea Gaza

Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio linalotaka kuchunguzwa kwa madai yote ya ukiukwaji wa sheria za kimataifa na za kibinadamu huko Gaza kuanzia tarehe 30 mwezi Machi mwaka huu.

Haki za wanawake Sudan zinatutia mashaka:UN

Ubaguzi na ukatili ikiwemo ukatili wa kingono dhidi ya wanawake na wasichana nchini Sudan umefanya macho yote ya ulimwengu kuikodolea nchi hiyo hasa kutokana na kesi ya msichana Noura Hussein Hammad Daoud.

Acheni kushambulia watoto- UNICEF

Watoto, wakati wote, wanahitaji amani na ulinzi, hiyo ni kauli iliyotolewa leo jijini New York, Marekani na Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia watoto la UNICEF, Henrietta H. Fore.

Mauritania mwachilieni mara moja mwandishi wa blog:UN

Kundi la wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa leo wameelezea hofu yao kuhusu kuendelea kushikiliwa rumande kwa mwandishi wa blogu wa Mauritania Cheikh Ould Mohamed M’kheitir kwa mdai ya kukiuka haki za binadamu.

Uamuzi wa mahakama Tanzania ni ushindi kwa umma- Balile

Nchini Tanzania hii leo Mahakama Kuu kanda ya Mtwara imezuia kwa muda kuanza kwa matumizi ya kanuni mpya za maudhui ya mtandao nchini humo.

Mambo ni magumu lakini tusikate tamaa- Mukajanga

Nchini Tanzania Baraza la Habari nchini humo, MCT, limesema maudhui ya mwaka huu ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari yamekuja wakati muafaka ambapo uhuru wa vyombo vya habari unabinywa kimataifa hadi kitaifa.