Mashambulio yaliotukia Ijumanne kwenye eneo la De Doorns, Afrika Kusini yaliochochewa na chuki na hofu dhidi ya wageni wa nchi, ikijumlisha raia wa Zimbabwe wenye kuomba hifadhi ya kisiasa, yaliripotiwa kusababisha baadhi ya wahamiaji 3,000 kukimibia mabanda waliokuwa wakijistiria ili kunusuru maisha, na ni kitendo ambacho kililaaniwa na Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR).
Shirika la UM juu ya Ulinzi Amani katika JKK (MONUC) limetangaza kukaribisha kukamatwa nchini Ujerumani, mnamo siku ya Ijumanne, kwa viongozi wawili wa kundi la waasi la FDLR (Forces démocratiques de Libération du Rwanda), wanaoitwa Ignace Murwanashyka and Straton Musoni.
Asubuhi Baraza la Usalama liliitisha kikao cha hadhara kuzingatia ripoti ya karibuni ya KM juu ya hali ya uharamia na ujambazi wa baharini unaotendeka kwenye mwambao wa Usomali.
Mahakama ya Kimataifa juu ya Rwanda (ICTR) imeamua kumwachia huru Hormisdas Nsengimana, aliyekuwa padri wa Rwanda, baada ya kuonekana hana hatia juu ya mashitaka ya kushiriki kwenye vitendo vya mauaji ya halaiki na makosa ya jinai dhidi ya utu na kuamrisha afunguliwe haraka kutoka Kituo cha UM cha Kuwekea Watu Kizuizini kiliopo Arusha, Tanzania.
Msemaji wa Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA), Elizabeth Byrs, aliwaambia waandishi habari Geneva, leo hii, kwamba hali ya usalama katika Kivu, Majimbo ya Oriental na Equateur katika JKK, bado inaendelea kuwa mbaya zaidi.
Ripoti mpya ya KM kuhusu hali ya uharamia na ujambazi katika mamlaka ya maeneo ya bahari ya mwambao wa Usomali, inayoambatana na Azimio 1846 la Baraza la Usalama, imechapishwa na kutolewa rasmi leo Ijumatatu, na imeeleza ya kuwa kuwepo kwa vyombo vya majeshi ya majini vya Mataifa Wanachama kwenye eneo hilo ni hatua muhimu iliosaidia kusawazisha utulivu wa mwambao wa Afrika Mashariki.
Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imeripoti ya kuwa vitendo vya uharamia na ujambazi mbaya uliofanyika katika wiki mbili zilizopita, kwenye maeneo ya mashariki katika Chad, ni hali inayohatarisha operesheni za kiutu za kunusuru umma muhitaji.
Kwenye ujumbe aliotuma Geneva katika Mkutano wa 2009 wa Mataifa Yalioidhinisha Mkataba wa Udhibiti Silaha Maalumu za Kawaida, KM Ban Ki-moon aliyahimiza Mataifa kuendelea kulenga majadiliano yao kwenye zile juhudi za kuimarisha hifadhi bora ya raia dhidi ya madhara yanayoletwa na matumizi ya silaha hizi katili na zisiobagua,