Sheria na Kuzuia Uhalifu

Waisraeli waliowashambulia wapalestina wawajibishwe-OHCHR

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, OHCHR imesikitishwa na vurugu za mashambulizi ya muda mrefu dhidi ya wapalestina ikirejelea shambulizi la hivi karibuni katika kijiji cha Al Mughayyir kilichoko katika ukingo wa magharibi wa mto Jordan.

Tafadhali Msumbiji mwachieni huru mwanahabari Amade Abubacar

Watalaamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa hii leo mjini Geneva Uswisi wamezitaka mamlaka nchini Msumbiji kumwachia mara moja mwanahabari Amade Abubacar na pia tuhuma kuwa ametendewa vibaya zichunguzwe.

Umoja wa Mataifa walaani vikali tukio la kigaidi mjini Bogota Colombia.

Katiku Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani vikali shambulio la bomu katika chuo cha polisi mjini Bogota nchini Colombia. Kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wake Stéphane Dujarric jijini New York, Marekani, Guterres ametuma pia salamu zake za rambirambi kwa familia za waathirika wa shambulio hilo la jana Alhamisi na akawatakia ahueni ya haraka wote waliojeruhiwa katika tukio hilo la bomu lililotegwa katika gari na kusababisha vifo vya takribani watu 21 na makumi walijeruhiwa.

Tunalaani tukio la Ugaidi nchini Kenya -Baraza la Usalama.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hii leo mjini New York Marekani limelaani vikali shambulizi la kigaidi lililotekelezwa jana tarehe 15 Januari mjini Nairobi Kenya na kusababisha vifo vya watu 14 na majeruhi.

Espinosa ataja vipaumbele vyake mkutano 73 ukibakiza miezi 8

Ikiwa imesalia miezi nane kabla ya kumalizika kwa mkutano wa 73 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, hii leo Rais wa baraza hilo, Maria Fernanda Espinosa amezungumza na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa na kueleza vipaumbele saba atakavyozingatia wakati wa kipindi hicho.

MICT yashukuru Tanzania kwa mafanikio iliyoyapata

Rais wa taasisi ya kimataifa inayoshughulikia masuala yaliyosalia ya makosa ya jinai,MICT  jaji Theodor Meron leo ameshukuru serikali ya Tanzania kwa msaada wake kwa taasisi hiyo wakati akitoa hotuba yake kwenye Kongamano la Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam.

Guterres akataa katakata serikali ya Guatemala kusitisha shughuli za CICIG

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amekutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Guatemala Sandra Jovel ambapo waziri huyo amemkabidhi Katibu Mkuu barua ya kumwarifu dhamira ya serikali ya Guatemala, kuvunja ya ndani ya saa 24 mkataba unaoanzisha kamisheni ya kimataifa dhidi ya ukatili nchini Guatemala CICIG.