Sheria na Kuzuia Uhalifu

Kusini mwa Afrika waongezeka vita dhidi ya ukatili:UNODC

Katika juhudi za kusaidia vyombo vya sheria Kusini mwa Afrika kukabiliana na ukatili wa kijinsia ofisi ya Umoja wa Mataifa ya madawa na uhalifu UNODC leo imesema imezindua muongozo na muhula wa mafunzo ili kuimarisha uwezo wa majeshi ya polisi katika kanda hiyo kukabiliana na ukatili huo.

Mkutano kulinda mali asili kufanyika Kinshasa DRC

Umoja wa Mataifa pamoja na serikali ya Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo watafanya mkutano juma lijalo kujadili njia za kulinda sehemu tano zilizo kwenye orodha ya sehemu za kiasili duniani ambazo ziko kwenye hatari ya kuangamia.

Haki za wapiga kura ziheshimiwe Sudan:Navi Pillay

Zikiwa zimesalia siku mbili kabla ya wananchi wa Sudan Kusini kuanza kupiga kura ya maoni ya kuamua hatma yao hapo siku ya Jumapili ijayo, mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay ameutaka uongozi wa Sudan kuhakikisha kura ya maoni inakuwa huru na ya haki.

Ban na Rais wa Jamuhuri ya Korea wajadili hali katika eneo hilo

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon na Rais wa Jamhuri ya watu wa Korea wamejadili hali ya sasa kwenye rasi ya Korea.

Uhalifu wa mtandao unatoa changamoto katika sheria:EU

Dunia hivi sasa imeelezwa kutegemea sana tekinolojia ya mawasiliano na mfumo wa bank umesema muungano wa Ulaya.

Mkuu wa haki za binadamu auasa utawala wa Ivory Coast

Juhudi za Kidiplomasia za viongozi wa nne wa Afrika zimeshindwa kutatua mvutano wa kisiasa nchini Ivory Coast ambapo Rais Laurent Gbagbo amegoma kuachia ngazi na kumpisha mpinzani wake Alassane Ouattara ambaye ametangaza kuwa muda wa upatanishi na majadiliano umekwisha.