Sheria na Kuzuia Uhalifu

Mashitaka dhidi ya mauaji ya Hariri yawsilishwa rasmi

Mwendesha mashitaka mkuu wa mahakama maalumu ya Lebanon Daniel Bellemare amewasilisha mashitaka rasmi ya washukiwa wa mauji ya aliyekuwa waziri mkuu wa Lebanon Rafiq Hariri.

Utawala wa sheria urejeshwe mara moja Tunisia:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo ameelezea hofu yake juu ya kuendelea kwa machafuko yanayosababisha kupotea kwa maisha ya watu nchini Tunisia,na ametoa wito wa kufanyika kwa mazungumzo kwa pande zote ili kumaliza tofauti zao kwa njia ya amani n kurejesha utulivu nchini humo.

Wafanyikazi wahamiaji wana wajibu mkubwa kwa nchi za magharibi:IOM

Ripoti mpya kuhusu wajibu wa wafanyikazi wahamiaji wanaofanya kazi za kuangalia watu wazee inasema kuwa watu wazee wanaweza kuwa changamoto kubwa kwa mataifa ya magharibi yaliyostawi hususan kupitia huduma zinazohitajika kuangalia idadi inayoendelea kuongezeka ya watu wazee.

Israel yaenendelea kukiuka sheria Ukingo wa Magharibi: UM

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa Richard Falk ameelezea hisia zake na kuvitaja kama ukiukaji wa sheria vitendo vya Israel kwenye ardhi inayoikalia kwenye ukingo wa magharibi vikiwemo vya mauaji ya wapalestina wanne wiki mbili zilizopita.

UM kuchunguza mauaji ya watu nchini Tunisia

Tume ya kutetea hali za binadamu ya Umoja wa Mataifa inasema kuwa iko tayari kushiriki kwenye uchunguzi kuhusiana na mauaji yanayokisiwa kufanyika nchini Tunisia wakati wa maaandamano juma hili.

Watu 247 wauawa kufuatia mzozo wa kisiasa Ivory Coast:UM

Tume ya kutetea haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa inasema kuwa idadi ya watu waliouawa nchini Ivory kufuatia kuzuka kwa mzozo wa kisiasa imeongezeka na kufikia 247 .

UNHCR na tume ya ulaya wanazuru Yemen kutathmini hali ya wakimbizi wa ndani

Kamishina mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR bwana Antonio Guterres na kamishina wa tume ya muungano wa Ulaya ya ushirikiano wa kimataifa, msaada wa kibinadamu na kukabili majanga Kristalina Georgieva wamewsili Yemen leo katika ziara yao ya kwanza ya kikazi pamoja.

Wanajeshi wa serikali DR Congo wakamatwa kwa ubakaji

Wanajeshi takribani 11 wa jeshi la serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamekamatwa wakishukiwa kujihusisha na ubakaji na uporaji kwa mujibu wa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo MONUSCO.

Wafanyikazi wa WFP watekwa nyara Darfur Sudan

Wafanyakazi watatu wa ndege wanaofanya kazi na mpango wa Umoja wa Mataifa wa chakula duniani WFP wametekwa nyara kwenye jimbo la Darfur Sudan.

UM walaani bughudha dhidi ya walinda amani wake Ivory Coast

Umoja wa Mataifa umelaani bughudha waliyofanyiwa wanajeshi wake wa kulinda amani nchini Ivory Coast UNOCI.