Sheria na Kuzuia Uhalifu

UNODC kuhusu juhudi za UM za kukomesha uhalifu wa mipangilio

Wiki hii tutaendelea na taarifa zetu kuhusu juhudi za UM katika kukomesha uhalifu wa mipangilio, ambao huhatarisha usalama na amani ya umma wa kimataifa.

UNODC imewakilisha ripoti mpya kuhusu biashara ya magendo ya kuchuuza watu wanaotoroshwa

Shirika la UM juu ya Udhibiti wa Madawa ya Kulevya na Uhalifu (UNODC) limewasilisha "Ripoti ya Dunia juu ya Utoroshaji Magendo wa Watu kwa 2007 - 2008".

UNODC inahimiza utawala bora Afrika Mashariki

Ofisi ya UM juu ya Udhibiti wa Madawa ya Kulevya na Uhalifu (UNODC) imeripoti kuibuka mkondo mkali wa uhalifu wa mpangilio, ulionekana kushtadi kwenye mataifa yaliopo ukanda wa Afrika Mashariki. Mkondo huu unahitajia kudhibitiwa mapema kabla haujasambaa zaidi kieneo na baadaye kuhatarisha usalama, inasema UNODC.

Mwendesha mashitaka wa kesi ya Taylor ametangaza kukamilisha ushahidi

Stephen Rapp, Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Mahakama Maalumu juu ya Jinai ya Vita katika Sierra Leone kwenye mahojiano ya Ijumatatu, na waandishi habari, hapa Makao Makuu alisema ya kwamba upande wa mashitaka umemaliza kuwasilisha ushahidi wa kesi dhidi ya Charles Taylor, aliyekuwa Raisi wa taifa jirani la Liberia.

ICTR imethibitisha tena kifungo cha maisha kwa mtuhumiwa Karera

Mahakama ya Rufaa ya Mahakama ya UM juu ya Rwanda (ICTR) imethibitisha tena kifungo cha maisha kwa mtuhumiwa François Karera, ambaye mnamo 07 Disemba 2007 alipatikana na hatia ya kushiriki kwenye mauaji ya halaiki, pamoja na maangamizi dhidi ya raia wenye jadi ya Kitutsi katika sekta ya Nyamirambo, wilaya ya Kigali Ville, na mauaji katika Kanisa la Ntarama mnamo 15 Aprili 1994, na pia kushiriki kwenye jinai dhidi ya utu iliofanyika katika kijiji cha Rushahi, kwenye Wilaya ya Kigali.