Sheria na Kuzuia Uhalifu

Mtoro wa pili wa makosa ya jinai ya halaiki Rwanda ametiwa mbaroni na ICTR

Ofisi ya Msemaji wa KM imeripoti kukamatwa kwenye mji wa Kampala, Uganda kwa Idelphonse Nizeyimana, aliyeshtakiwa na Mahakama ya Kimataifa juu ya Rwanda (ICTR) kushiriki kwenye mauaji ya Watutsi na Wahutu wenye siasa za wastani nchini Rwanda katika 1994.

Jumuiya ya kimataifa yalaani mauaji ya watumishi wa UM Islamabad

Ijumatatu mchana, kwenye mji wa Islamabad, Pakistan watumishi watano wa UM wanaofanya kazi na Ofisi ya UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) waliuawa baada ya kufanyika shambulio la bomu la kujitolea mhanga kwenye jengo lao, tukio ambalo vile vile lilisababisha makorja ya majeruhi, baadhi yao wakiwa katika hali mbaya kabisa na ambao hivi sasa wanapatiwa matibabu hospitali.

Siku ya Kimataifa ya Kutotumia Nguvu wala Mabavu

Hii leo UM unaadhimisha Siku ya Kimataifa Dhidi ya Matumizi ya Nguvu. Risala ya KM juu ya siku hii imetoa mwito maalumu unaoutaka umma wote wa kimataifa kuiadhimisha siku hiyo kwa kukumbushana urithi wa kimaadili wa Mahatma Gandhi ambaye aliwahimiza walimwengu kutatua mifarakano yao kwa taratibu za amani, zisiotumia nguvu, mabavu wala fujo.

Mapigano mapya Usomali huathiri zaidi raia, kuhadharisha UNHCR

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limeripoti mfumko wa mapigano ya karibuni katika jimbo la Kati-Kusini la Usomali yamechochea tena wimbi la wahamiaji wapya wa ndani walioamua kuelekea maeneo jirani kutafuta hifadhi.