Sheria na Kuzuia Uhalifu

Mkariri wa UM anayetetea haki za wateswa amefukuzwa Zimbabwe

Manfred Nowak, Mtaalamu wa UM juu ya masuala ya mateso, na vitendo vyengine visio vya kiutu vyeye kudhalilisha hadhi ya ubinadamu, alkhamisi alitangaza, kutokea Johannesburg, Afrika Kusini ya kuwa ana wasiwasi juu ya madai ya kuwepo hali mbaya, iliokiuka haki za kiutu za wafungwa, katika magereza ya Zimbabwe, taarifa aliowakilisha saa 24 baada ya kunyimwa ruhusa ya kuingia nchini humo kuendeleza uchunguzi kuhusu madai hayo.

Hapa na pale

KM amemteua Dktr. David Nabarro kuwa Mjumbe M aalumu juu ya Udhibitaji Bora wa Lishe na Chakula duniani. Jukumu la Dktr. Nabarro hasa litakuwa ni kumsaidia KM kuhimiza mataifa kutumia miradi ya kizalendo ya kujitegemea chakula maridhawa na udhibiti bora wa lishe, kwa kufuata taratibu za jumla, zenye malengo yalioratibiwa kujumuisha kipamoja mchango muhimu wa mashirika ya kimataifa, ili kukuza misaada inayohitajika kutekelza huduma hizo kwa mafanikio. Tangu mwezi Januari mwaka huu, Dktr. Nabarro alidhaminiwa madaraka ya kushughulikia masuala yanayohusu chakula, na kuandaa taratibu za kuimarisha akiba ya chakula duniani kwa madhumuni ya kutosheleza mahitaji ya umma wa kimataifa.

Serikali ya Zimbabwe imemnyima Mkariri wa Haki za Bindamu ruhusu ya kuingia nchini

Serikali ya Zimbabwe imeripotiwa kuzuia ziara ya Manfred Nowak, mtaalamu wa UM juu ya masuala yanayohusu mateso, na vitendo vyengine visio vya kiutu vinavyodhalilisha hadhi ya ubinadamu.

ICTR imeanzisha warsha wa mafunzo maalumu kwa walimu na wanafunzi kuhusu shughuli zake

Ijumanne ya tarehe 27 Oktoba 2009, Mahakama ya Kimataifa juu ya Rwanda (ICTR) imeanzisha, kwa mara ya kwanza, Warsha Maalumu wa kuwahusisha walimu na wanafunzi wa skuli za sekandari kutoka wilaya za Rulindo na Musanze, ziliopo Rwanda Kaskazini,

Mahakama Maalum juu ya Makosa ya Vita katika Sierra Leone imekataa rufaa ya wahukumiwa waasi wa RUF

Hukumu ya mwisho ya Mahakama Malumu juu ya Makosa ya Vita katika Sierra Leone, imeidhinisha adhabu iliopitishwa kabla, dhidi ya viongozi watatu wa kundi la waasi la RUF, iendelee kutekelezwa kwa kulingana na makosa waliotuhumiwa nayo, ikijumlisha makosa ya kufanyisha ndoa za kulazimishwa, kitendo ambacho kilitafsiriwa kuharamisha ubinadamu, na vile vile yale makosa ya kuhujumu walinziamani wa kimataifa - na hii ni mara ya kwanza kwa mahakama za kimataifa kuchukua hatua hii ya kisheria. Mahakama ya Maalumu ya Sierra leone ilikataa kabisa maombi yote ya rufaa ya washtakiwa, isipokuwa ombi moja la mtuhumiwa Agustine Gbao, ambaye hapo kabla alishtakiwa kuendeleza adhabu za jamii, hukumu ambayo ilibatilishwa. Hata hivyo, Gbao ataendelea kutumikia kifungo cha miaka 25 gerezani.

Mahakama ya ICC inazingatia matukio ya karibuni Guinea

Luis Moreno-Ocampo, Mwendesha Mashitaka wa Mahakama ya Kimataifa juu ya Makosa ya Jinai ya Halaiki (ICC) leo amenakiliwa akithibitisha ya kuwa Ofisi yake imeanzisha uchunguzi maalumu kuhusu tukio la Guinea, ambapo mwezi iliopita waandamanaji wa upinzani, wanaokadiriwa 150 waliuawa huko na vikosi vya usalama, pale walipokusanyika kwenye mkutano wa hadhara.

Aliyekuwa ofisa wa upelelezi Rwanda kukana mashtaka ya Mahakama ya ICTR

Idelphonse NIZEYIMANA, aliyekuwa ofisa wa idara ya upelelezi katika Rwanda, amekana makosa ya kushiriki kwenye mauaji ya halaiki pale alipohudhuria Ijumatano Mahakama ya Kimataifa juu ya Rwanda (ICTR), kuandikisha jibu la kesi alioshtakiwa na mahakama hiyo.

Udhalilishaji dhidi ya wanawake bado waendelezwa kwenye maeneo ya mapigano, atahadharisha ofisa wa kamati ya CEDAW

Naéla Gabr, mwenyekiti wa kamati inayosimamia utekelezaji wa Mkataba wa UM Kuondosha Aina Zote za Ubaguzi Dhidi ya Wanawake (CEDAW) Ijumatatu alipohutubia Baraza Kuu aliwaeleza wajumbe wa kimataifa kwamba vitendo vya unyanyasaji na udhalilishaji katili wa wanawake walionaswa kwenye mazingira ya mapigano bado umeselelea duniani,

Ripoti ya mwaka ya UNICEF juu ya hifadhi ya watoto imesisitiza bidii zaidi zahitajika kuwalinda watoto dhidi ya udhalilishaji

Ripoti ya mwaka ya UNICEF kuhusu hifadhi ya watoto kimataifa imeeleza kwamba licha ya kuwa karibuni kulipatikana maendeleo kwenye suala hilo, watoto bado wanaendelea kudhalilishwa na kukabiliwa na vitendo karaha kadha wa kadha dhidi yao.

BU lashauriana kuzingatia barua ya Libya juu ya ripoti ya Tume ya Goldstone kuhusu Ghaza

Alasiri, Baraza la Usalama lilikutana kushauriana juu ya barua iliotumiwa na Ubalozi wa Kudumu wa Libya katika UM, barua ambayo ilipendekeza kuitishwe kikao cha dharura, kuzingatia ripoti ya ile tume ya kuchunguza ukweli juu ya mashambulio ya Tarafa ya Ghaza yaliotukia mwisho wa 2008 na mwanzo wa mwaka huu.